KAMBI YA MAISHA BORA AFYA BORA JUU YA UCHUNGUZI WA MAGONJWA MBALI MBALI KUANZA RASMI KESHO MICHEWENI .
Na, AMINA AHMED PEMBA.
WANANCHI wenye matatizo ya kiafya Kutoka maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kambi ya siku tano ya uchunguzi wa magonjwa mbali mbali itakayoanza rasmi kesho tarehe 8 katika viwanja vya Shaame Mata wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba ili kuweza kuchunguza afya zao bila malipo yeyote na kuweza kupatiwa matibabu .
SALAMA MBAROUK KHATIB -RC KASKAZINI.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo mbali mbali kupitia mkutano maalum na waandishi wa habari wa vyombo tofauti ulioandaliwa na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Faundation (ZMBF) huko katika ukumbi wa Micheweni mapema leo kuelekea uzinduzi maalum wa kambi hiyo itakayozinduliwa kwa bonanza maalum la maisha bora afya bora mapema kesho asubuhi .
Amesema Taifa bora ni lile ambalo wananchi wake wanakuwa na afya hivyo lengo la kambi hiyo ya siku tano inayotarajia kuchunguza afya za watu elfu 5 imedhamiria kurahisisha huduma ya uchunguzi wa magonjwa mbali mbali .
Aidha Salama amewatoa hofu wananchi ambao wataweza kufika katika kambi hiyo amabao watabainika kuwa na magonjwa yeyote baada ya uchunguzi na kusema kuwa utaratibu wa rufaa kwajili ya matibabu utatolewa .
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amesema kuwa tayari maandalizi kwajili ya bonanza na kambi hiyo ya maisha bora afya bora ndani ya wilaya hiyo yamekamilika ikiwemo suala la kuimarisha ulinzi na usalama zaidi katika kutimiza malengo ya kambi hiyo.
Akitoa ufafanuzi juu ya kambi hiyo ya uchunguzi afisa mdhamini wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali amesema kuwa Madaktari bingwa wa magonjwa mbali mbali wanatarajiwa kuungana pamoja katika kambi hiyo ya siku tano .
KHAMIS BILAL ALI - MDHAMINI AFYA PEMBA.
Hata hivyo amewataka wananchi pia kuunga mkono zoezi la uchangiaji damu katika bonanza hilo .
Miongoni mwa huduma za uchunguzi zinazotarajiwa kutolewa katika kambi hiyo iliyoandaliwa na taasisi hiyo ya zanzibar maisha bora faundation
kwa lengo la kuondoa changamoto ya maradhi mbali mbali ni pamoja na huduma za uchunguzi wa X ray ,uchunguzi wa magonjwa ya Moyo, uchunguzi wa sitiscan, huduma uchunguzi meno,ngozi,macho na nyenginezo.
Mwisho.
WANANCHI wenye matatizo ya kiafya Kutoka maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kambi ya siku tano ya uchunguzi wa magonjwa mbali mbali itakayoanza rasmi kesho tarehe 8 katika viwanja vya Shaame Mata wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba ili kuweza kuchunguza afya zao bila malipo yeyote na kuweza kupatiwa matibabu .
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo mbali mbali kupitia mkutano maalum na waandishi wa habari wa vyombo tofauti ulioandaliwa na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Faundation ( ZMBF ) huko katika ukumbi wa Micheweni mapema leo kuelekea uzinduzi maalum wa kambi hiyo itakayozinduliwa kwa bonanza maalum la maisha bora afya bora mapema kesho asubuhi .
Amesema Taifa bora ni taifa ambalo wananchi wake wanakuwa na afya hivyo lengo la kambi hiyo ya siku tano inayotarajia kuchunguza afya za watu elfu 5 imedhamiria kurahisisha huduma ya uchunguzi wa magonjwa mbali mbali .
Aidha Salama amewatoa hofu wananchi ambao wataweza kufika katika kambi hiyo amabao watabainika kuwa na magonjwa yeyote baada ya uchunguzi na kusema kuwa
utaratibu wa rufaa kwajili ya matibabu utatolewa .
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amesema kuwa tayari maandalizi kwajili ya bonanza na kambi hiyo ya maisha bora afya bora ndani ya wilaya hiyo yamekamilika ikiwemo suala la kuimarisha ulinzi na usalama zaidi katika kutimiza malengo ya kambi hiyo.
Akitoa ufafanuzi juu ya kambi hiyo ya uchunguzi afisa mdhamini wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali amesema kuwa Madaktari bingwa wa magonjwa mbali mbaliwanatarajiwa kuungana pamoja katika kambi hiyo ya siku tano .
Hata hivyo amewataka wananchi pia kuunga mkono zoezi la uchangiaji damu katika bonanza hilo .
Miongoni mwa huduma za uchunguzi zinazotarajiwa kutolewa katika kambi hiyo iliyoandaliwa na taasisi hiyo ya zanzibar maisha bora faundation
kwa lengo la kuondoa changamoto ya maradhi mbali mbali ni pamoja na huduma za uchunguzi wa X ray ,uchunguzi wa magonjwa ya Moyo, uchunguzi wa sitiscan, huduma uchunguzi meno,ngozi,macho na nyenginezo.
Mwisho.
Comments
Post a Comment