EPA YAADHIMISHA SIKU YA ZIPASO KWA BONANZA LA AINA YAKE PEMBA TIMU YA WANAFUNZI YAIBUKA NA USHINDI .

Na - AMINA AHMED MOH'D,PEMBA.

TIMU ya chuo cha utawala wa umma EPA epa student  imeibuka kidedea katika mchezo wa  fainali ya mpira  wa miguu uliofanyika katika viunga vya uwanja wa Gombani kongwe Chake Chake Pemba ikiwa ni bonanza maalum la  maadhimisho  ya siku ya serikali za wanafunzi  ZIPASO day .
Fainali hiyo iliyochezwa kati ya wanafunzi wa chuo hicho pamoja  na  vijana kutoka timu ya mpira pesa Chake chake  ambapo kabla ya fainali hiyo  jumla ya timu  4 ziliumana kuutafuta ushindi  katika viwanja hivyo hapo jana  majira ya saa 10  jioni ambazo ni Epa student,Transfoma,Epa Staff pamoja na timu ya mpira Pesa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa fainali na michezo mbali mbali katika bonanza hilo Wakili wa Serikali  Kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Pemba Jecha Vuai Jecha ameipongeza zipaso kwa kuandaa boananza hilo kisiwani Pemba  ambapo amesema kuwa litasaidia kuongeza hamasa kwa vijana  na jamii  katika kujiunga na chuo hicho ambacho kinarudisha shukurana kwa kufanya kazi na kushiriki shughuli  mbali mbali  kwa wananjamii.
Akizungumza kwa upande wake mara baada ya kumalizika kwa  fainali hiyo iliyotanguliwa  na michezo na burudani mbali mbali  rais wa serikali ya wanafunzi  kutoka chuo cha utawala wa umma Epa  Najla Abdalla Mussa  amesema kuwa lengo la kuadhimisha siku hiyo ni  kuleta mashirikiano  ya pamoja kupitia michezo  kwa  wanafunzi  wa chuo hicho matawi mbali mbali unguja na Pemba .
  NAJLA  ABDALLA MUSSA- RAIS           SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA UTAWALA WA UMMA ZANZIBAR - EPA .
Aidha Najla  amesema kuwa kupitia bonanza hilo ni kuionesha  jamii uimara wa elimu zinazotolewa na  chuo hicho katika  kuisadia na kuhamasisha wanafunzi ambao wameshindwa kuendelea na masomo pamoja  ushiriki wa shughuli mbali mbali ikiwemo michezo.

Kwa upande wake  Afisa uhusiano wa chuo hicho  amewataka vijana wenye sifa za kujiunga na chuo hicho  kuwahamasisha vijana walioshiriki bonanza hilo pamoja na walioko katika maeneo mbali mbali  kujiunga na chuo hicho kwajili ya kupata kozi mbali mbali  zitakazowasaidia  kujiendeleza kiuchumi ambapo kwa sasa tayari udahili wa wanafunzi wapya umeanza.

Zawadi ya pesa taslim pamoja ja flana  kwa washindi wa mpira wa miguu ambao ni timu ya Epa student zimetolewa  huku washiriki wengine walioshiriki michezo kama  vile  mbio za magunia,kufukuza kuku,mashindano ya kukuna nazi, pamoja na kukimbia  zilitolewa uwanjani hapo ambapo kabla ya maadhimisho hayo ziposa  kutoka Epa pia waliwatembelea na kuwafariji  wazee  katika nyumba ya wazee Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mwisho .

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.