150 KUSHIRIKI RIADHA WAKIWEMO WANAFUNZI KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA TAREHE 29 MWEZI HUU
Siku ya Mtoto wa Afrika Zanzibar
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ)
kwa kushirikiana na Idara ya Michezo, Jumuiya ya Wanasheria Wanawake
Zanzibar (ZAFELA), Taasisi ya Maendeleo ya Mashirikiano ya Ujerumani (GIZ)
na Kituo cha Mijadala kwa Vijana (CYD), inatarajia kuadhimisha ya siku ya
kimataifa ya Mtoto wa Afrika tarehe 29 Juni 2024 kwa kuandaa mashindano
ya riadha kwa wanafunzi wa skuli mbalimbali za Zanzibar.
Maadhimisho hayo yatawahusisha jumla ya washiriki 150 ambapo kati ya hao
watakaoshiriki mashindano ni wanafunzi 75 kutoka katika skuli za Unguja
ambazo zimeshajiandaa kushiriki mashindano hayo.
Tukio hili muhimu ambalo linalenga kuhamasisha usawa wa kijinsia katika
michezo litawaleta pamoja wadau kutoka taasisi za kierikali na zisizokuwa za
kiserikali ikiwemo wanafunzi kutoka skuli mbalimbali za Unguja, wanamichezo,
walimu wa michezo, na wadau wote wa masuala ya usawa wa kijinsia.
Maadhimisho haya yanatoa fursa kwa wasichana kuonesha vipaji vyao na
uwezo wao wa kushiriki katika michezo mbalimbali, pamoja na kujadili
changamoto na vikwazo vinavyowazuia kushiriki katika michezo na kuhimiza
uanzishwaji wa madawati ya jinsia katika taasisi za michezo.
Mashindano haya ya riadha yataanza saa 12 na nusu asubuhi, yakianzia
maeneo ya Forodhani na yataishia katika viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar
yakishirikisha wanafunzi wa jinsia zote kutoka skuli mbalimbali za Unguja.
Kaulimbiu ya wadau katika maadhimisho ya mwaka huu ni “Wakati ni sasa!
Wekeza katika elimu na michezo kwa watoto wote”. Tukio hili
linatarajiwa kuleta mwamko na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa
kuwapa nafasi sawa watoto wote kushiriki katika michezo, bila kujali jinsia zao.
Mashindanohayoyatatoawashindiwatatuzaidiwanawakenawatatu
wanaume na kutambuliwa rasmi.
Tunaamini kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kuleta usawa wa kijinsia na
kuwawezesha watoto wa kike na wa kiume kujifunza stadi za maisha, kujenga
ujasiri, na kushirikiana kwa amani na kuheshimiana.
Tunawaalika wanahabari, wazazi, walezi, na wananchi wote kujitokeza kwa
wingi kushuhudia na kuunga mkono tukio hili la kihistoria katika kukuza usawa
wa kijinsia na kuwawezesha watoto wote kufikia ndoto zao katika Nyanja
mbali mbali bila vizuizi vyovyote.
#TamwaZanzibar
#MichezoKwaMaendeleo.
Comments
Post a Comment