Wazazi wacheni Mila potofu kuibua vipaji vya michezo Kwa watu wenye ulemavu
Wazazi na walezi kisiwani Pemba wametakiwa kuacha tamaduni na Mila potofu zinazorejesha nyuma ndoto za wanafunzi wasichana wenye ulemavu kushiriki kwenye michezo.
Ameyasema hayo mratibu wa idara ya michezo na utamaduni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mzee Ali Abdallah wakati akizungumza na mwandiahi wa Habari hizi huko ofisi kwake ChakeChake.
Amesema Bado jamii Haina mwamko kwa wasichana mashuleni hususani wenye ulemavu kuwapa uhuru wa kushiriki kwenye michezo Hali inayopelekea kundi hili kutotimiza ndoto zao kwani kwa sasa sanaa ni kiwanda cha michezo.
Ameongeza, ni vyema jamii kufahamu kwa sasa wizara imeandaa tamasha maalum la michezo kwa wenye ulemavu hivyo ni vyema kuwaacha wanafunzi wa kike wa kundi hili kutumia fursa hiyo.
Nao baadhi ya wazazi wameiomba wizara kuandaa Mazingira rafiki yatakayowawezeaha wanawake wenye ulemavu kushiriki bila vikwazo kwani Mazingira kwa sasa hayaridhishi.
Nae Khamis Hamad Juma Kaimu Mkuu wa Idara ya Michezo Pemba, amesema wizara ina Mipango yakujenga viwanja vya kisasa kwa skuli maalum vitakavyowawezeaha wanafunzi kushiriki michezo minne kwa kiwanja kimoja hivyo ni vyema wazazi , walezi na walimu kutumia fursa hiyo Ili kuibua vipi vya wanafunzi wa kike maskulini.
Kwa upande wake Nashfa Ali amesema mbali na hatua zinazochukiliwa na wizara ila Bado Kuna changamoto kwa wasichana wenye ulemavu Hali inayopelekea kukatisha ndoto zao za kua wanamichezo vinara.
Kwa upande wake Mashavu Juma Mabrouk mratib barz la watu wenye ulemavu Pemba amesema wakati umefika kwa sasa wazazi kubadili mitazamo Yao , kufanya hivyo kutasaidia wasichana wenye ulemavu kushinda tunzo kwenye michezo na kujikwamua kimaisha.
Jumla ya skuli tatu kwa upande wa Pemba zinatarajiwa kujengwa viwanja vya kisasa vya michezo Hali itakayosaidia kutoachwa nyuma kwa wanafunzi wa kike.
Comments
Post a Comment