PEMBA PRESS CLUB YAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MATTAR AWATOA HOFU AAHIDI MASHIRIKIANO ZAIDI KWA WAANDISHI.

NA , AMINA AHMED  MOH'D- PEMBA.

UONGOZI wa Mkoa Kusini Pemba umesema utaendelea kutoa mashirikiano kwa waandishi wa habari kisiwani humo ili kuweza kurahisisha utendaji wa  kazi zao za kila siku na kuleta mabadiliko katika jamii juu ya mambo mbali mbali.

Kauli hiyo imetolewa  na mkuu  wa  mkoa huo  Mattar Zahor Massoud  alipokuwa akifungua mkutano maalum wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari uliandaliwa  na Club ya waandishi wa Habari Pemba  ( PPC )  uliofanyika katika ukumbi wa Samail Gombani Chake Chake mapema leo .

Amesema  maelezo na ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali  yanayohusu maendeleo ya wananchi yanaweza kufikiwa  iwapo waandishi wenyewe kisiwani humo watakuwa tayari kuitumia fursa hiyo ya mashirikiano  katika kutafuta taarifa kutoka kwa vyanzo sahihi .

Aidha  mkuu huyo akaitumia nafasi hiyo kuwataka waandishi wa habari  kuandika habari zitakazoelimisha jamii juu ya kuhifadhi mazingira kwa nadharia ya kutunza urithi wa kijani  sambamba na habari zitakazobadilisha jamii juu ya suala hilo  katika hatua za awali.

 Mattar akatumia fursa hiyo pia kuwaasa waandishi wa habari kisiwani humo  kujiendeleza zaidi kielimu  ili kujiongezea fursa na maarifa katika kutenda kazi ya habari kwa ufanisi na uweledi.

Amesema iwapo waandishi wataendelea kuongeza ujuzi katika taaluma hiyo kutasaidia jamii kuweza kuwatofautisha waandishi wenye uweledi na makanjanja wanaovamia  tasnia hiyo na kuwaharibia sifa zao kwa kukiuka maadili ya habari.

Kwa upande wake Afisa mdhamini wa  wizara  ya habari  Pemba Mfamau Lali Mfamau  amewataka waandishi wa  habari  hao ambao ni wanachama wa Pemba Press Club kuendelea kusimamia nidhamu  na kutojihusisha kuwa sehemu ya kuvunja nidhamu zilizowekwa na taasisi zinazosimamia  tasnia hiyo.

Akizungumza  Katika Mkutano wa maadhimisho hayo yaliobeba  ujumbe wa Uandishi wa habari kwa Mabadiliko ya Tabia ya nchi Mwenyekiti wa Pemba Press Club PPC  Bakar Mussa Juma amesema  wanachama wa  club hiyo wataendelea kushirikiana na taasisi yeyote katika  kuleta maendeleo kwa wananchi juu ya mambo mbali mbali.


 Tamati ya maadhimisho hayo mwaka huu  wanachama wa club  hiyo wanatarajiwa  kupanda miti katika eneo la Kambini kichokochwe ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono  utunzaji wa mazingira  na kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.


Mwisho.








Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.