MRAJIS ASASI ZA KIRAIA ZANZIBAR AWAPONGEZA WANAVIKUNDI SHIRIKISHI
NA , AMINA AHMED MOH'D.
MRAJIS wa asasi za kiraia Zanzibar Ahmed Khalid amewaasa wana vikundi jumuishi vya ushirika wa kukopa na kuweka kisiwani Pemba kuendeleza umoja na mashirikiano katika kutatua changamoto mbali mbali na kusaidia kutimiza malengo yao waliyojiwekea katika kujiendeleza kiuchumi bila kuwa na utegemezi .
Ametoa wito huo leo alipokuwa akizungumza na wana vikundi wa aina mbali mbali Ole, Mvumoni pamoja na Mbuzini wilaya ya Chake chake katika ziara maalum ya kukagua vikundi vya uwezeshaji kiuchumi kwa watu wenye ulemavu (Kijaluba isave ) ikiwa ni utekelezaji wa mradi jumuishi wa kuwawezesha watu wenye ulemavu kiuchumi ambayo imeandaliwa na shirikisho la jumuia za watu wenye ulemavu zanzibar Shijuwaza.
Amesema changamoto zinazojitokeza katika vikundi hivyo zinaweza kupata ufumbuzi iwapo wanavikundi hao watakuwa na mashirikiano ya pamoja katika kuzalisha fikra za pamoja zitakazobadilisha changamoto kuwa fursa za kimaendeleo.
Aidha mrajis huyo amewapongeza wanavikundi hao kwa kuendelea kufikia malengo ya mradi wa kijaluba isave kujiwezesha kiuchumi bila utegemezi kwa watu wenye ulemavu .
Hata hivyo amesema kuwa wataendelea kuzisemea changamoto mbali mbali zinazowakabili katika kuendesha vikundi hivyo ikiwemo kukosa fedha ili kupatiwa ufumbuzi.
Wakizungumza na wanaushirika hao mwenyekiti wa shijuwaza Mwan - dawa Khamis pamoja na mjumbe wa bodi shijuwaza Joseph Abdalla Meza wamesema kuwa Jumuia hiyo i5a3ndelea kuwa mstari wa mbele katika kuona watu wenye ulemavu wanapewa kipaumbele katika shughuli za maendeleo.
Akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya mradi huo Msaidizi afisa mradi kijaluba isave Upande wa Pemba Aisha Abdalla Juma amesema kuwa mwaka mmoja wa majaribio katika mradi huo wa majaribio umefanikiwa kufikia malengo yaliokusudiwa ya kuweza kujisimamia wenyewe katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo.
Amesema miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa katika mradi huo ni kuwaweka pamoja watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu kushirikiana pamoja katika kujiwekea hakiba na kuweza kupata mikopo ya kuweza kufanya shughuli zao za kujitegemea kiuchumi.
Nao baadhi ya wanavikundi hao akiwemo said Omar Said wameishukuru shijuwaza na Tamwa kwa kusimamia mradi huo wa Kijaluba isave ambao umewaletea mabadiliko katika kujikomboa kiuchumi ikiwemo kubadilika kiakili katika kujitegemea wenyewe watu wenye ulemavu kiakili.
Mradi huo wa majaribio kwa wanaushirika umekusanya jumla ya shilingi milioni 54 laki moja elfu tisini 800 ambapo vikundi 21 katika maeneo mbali mbali ya shehia hizo tatu vimefanikiwa kuendesha shughuli zao ikiwemo kukopeshana fedha na kuanzisha biashara mbali mbali ambapo asilimia 60 ya wanachama wa vikundi hivyo ni watu wenye ulemavu .
Comments
Post a Comment