MICHE 10000 YA MIKOKO YAPANDWA KAMBINI PPC WAUNGANA NA WANANCHI KUDHIBITI UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

Na,Amina Ahmed Moh'd Pemba.
WANACHAMA  wa Club  ya waandishi wa habari Pemba ( PPC ) wakishirikiana   na Wanakijiji wa Kambini Kichokochwe pamoja na  jumuia ya  Community Forest Pemba  ( CFP ) wameshiriki zoezi la upandaji wa miche  aina ya mikoko ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo habari duniani.


 Zoezi la   upandaji wa miche hiyo limefanyika  mapema leo katika bahari ya Kambini  Kichokochwe  Mchanga Mdogo wilaya ya Wete  mkoa wa Kaskazini Pemba  ambayo ni moja kati ya maeneo 200  kisiwani humo   yaliy𝕠𝕙𝕒𝕣𝕚𝕓𝕚𝕨𝕒  na mabadiliko ya tabia ya nchi   kutokana na  ukataji wa   miti  hiyo kiholela kwajili ya matumizi mbali mbali.
 
Awali akizungumza kwa niaba ya wanachama hao ambao ni waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali  kutoka kisiwani humo mwenyekiti wa club hiyo Pemba Bakar Mussa Juma  amesema lengo la kuadhimisha siku hiyo kwa kushiriki zoezi hilo la upandaji wa miche ya mikoko ni kusaidia kuendeleza kukabiliana na athari za kimazingira  zinazopelekea kuleta mabadiliko ya tabia ya nchi.

Aidha Mwenyekiti huyo ameishukuru CFP kwa kukubali kuwaunga mkono katika kufanikisha zoezi hilo la upandaji wa miche ya mikoko katika bahari hiyo ya kichokochwe ambapo amesema  itakapokuwa itasaidia kudhibiti  kupanda kwa maji ya bahari katika maeneo  ya makazi ya watu .

Kwa upande wake mwenyekiti wa CFP Kombo Seif Khamis  ameishukuru club ya waandishi wa habari Pemba PPC kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira ambapo amewataka  kuendelea kuelimisha jamii kupitia vyombo vya habari vyao umuhimu wa kutunza mazingira na kupanda miti huku akizitaka club  wananchi  na wadau wengine mbali mbali kuiga mfano huo uliotolewa na PPC.
 Nao baadhi ya  wanakijiji wa Kambini kichokochwe   wameishukuru  Club hiyo kwa kwa kujitolea juu ya suala hilo katika kijiji chao ambapo amesema licha ya juhudi mbali mbali wanazoendelea kuzichukua ikiwemo kupiga matuta kudhibiti maji ya chumvi kusogea katika maeneo ya wananchi lakini bado yamekuwa yakiwaletea athari mbali mbali hivyo upandaji wa miche hiyo  kutasaidia kukabiliana na athari zinazojitokeza ikiwemo kuharibika kwa mashamba yao  kutokana maji ya bahari  yanayoendelea kusogea siku hadi siku katika maeneo yao.

 Akitoa ufafanuzi juu ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi   Mbarouk Mussa kutoka CFP amesema ni vyema jamii ikaendelea  na utaratibu wa upandaji wa miti kwani kutasaidia kupunguza athari mbali mbali ikiwemo kuongezeka kwa joto sambamba na kuhuisha urithi wa kijani kama ambavyo serikali inataka  .

Katika Zoezi hilo Jumla ya miche ya Mikoko elfu 10000  imepandwa katika eneo la bahari hiyo ya Kichokochwe ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono  juhudi za serikali ya Mapinduzi ya zanzibar  pamoja na wadau mbali mbali wa mazingira dunianin katika  kukabiliana na athari zinazotokana na    mabadiliko ya tabia ya nchi .

Mwisho.


Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.