KAMBI YA WIKI 3 JUU YA UCHUNGUZI WA SARATANI YA SHINGO YA MLANGO WA KIZAZI KWA KINA MAMA KISIWANI PEMBA YAZINDULIWA RASMI LEO AKINA MAMA WAASWA KUJITOKEZA .

AMINA AHMED MOH'D 
 WANANCHI kisiwani  Pemba  wametakiwa kujitokeza kwa wingi  katika  kambi za uchunguzi  wa  saratani ya shingo ya mlango wa kizazi zilizofunguliwa  tena leo kisiwani humo  ili kuweza kuchunguzwa afya  zao  na watakaobainika  kuweza kupatiwa matibabu  dhidi ya ugonjwa huo kwa kufuata utaratibu maalum  wa utolewaji wa huduma hizo uliowekwa na madaktari  katika wilaya  zote nne .

Kambi  hiyo ya madaktari  36  kutoka  Jasmin Clove nchini China  kwa kushirikiana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar  ambayo imedhamiria kutoa huduma hizo kwa makundi  maalum ya wanawake ambao ni wenye umri kati ya miaka 19 hadi  69   kutoka maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba  lengo ikiwa ni kusaidia jamii  ya wanawake na wasichana kisiwani humo kuwa na afya bora.
 Kauli hiyo imetolewa na Afisa mdhamini wizara ya nchi ofisi ya rais  kazi uchumi na uwekezaji Pemba Fadhila Hassan Abdalla alipokuwa akizungumza na akina mama kutoka maeneo mbali mbali waliofika katika hospitali ya Chake chake katika ufunguzi wa kambi hiyo ya uchunguzi  ambayo inatarajiwa kutoa huduma hizo kwa muda wa wiki 3 katikamaeneo mbali mbali  ya hosptali ikiwemo Abdalla Mzee  Wete, Micheweni pamoja na chake chake.

Akizungumza kwa niaba ya  madaktari hao   mkuu wa kambi hiyo  Xiaomin  Qi  kutoka  kampuni ya Jasmine clove amesema kuwa  lengo  la kuweka kambi hiyo kisiwani Pemba   ni  kusaidia kutoa huduma ya matibbu kwa akina mama kutokana na kuwepo kwa uhitaji mkubwa katika suala hilo . 

Kwa upande wake afisa mdhamini  wizara ya afya Pemba ameishukuru  serikali ya china  kwa kuendelea kutoa mashirikiano na wizara ya afya katika kusaidia kuimarisha huduma za matibabu mbali mbali  kisiwani pemba ikiwemo suala hilo la uchunguzi wa magonjwa dhidi ya saratani ya shingo ya mlango wa kizazi. 
Kambi  hiyo ya wiki 3  kisiwani   humo   inatarajiwa kutoa huduma  hizo za uchunguzi kwa wanawake Zaidi   ya  wagonjwa  elfu 34 miatano  ambapo  hadi kufikia awamu hii ya 6   ya utekelezaji wa mradi huo   wagonjwa 2 elfu 20 tayari wameshafanyiwa uchunguzi  huku  wagonjwa elfu 3000 wakionekana kuwa na  magonjwa mbali mbali  huku 561 wakigundulika kuwa na saratani ya shingo ya mlango wa kizazi kwa  hatua za  awali  na wagonjwa 72 wakigundulika kuwa na ugonjwa huo katioka hatua ya 3.

MWISHO.


Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.