EKWADEO WAASWA KUIFANYIA KAZI ELIMU WALIYOPATIWA ILI KULETA MABADILIKO.
VIONGOZI na wanachama wa Jumuiya ya Elimu Kwanza Development Organization wametaiwa kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku moja mkuu wa kituo cha polisi wete Ayoub Ramadhan Abdalla amesema ili kuleta mabadiliko katika jamii ni vyema kwa viongozi na wanachama hao kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili waweza kuibua changamot zilizomo katika jamii na kusaidia serikali katika kupambana na Watoto waliojiingiza katika vikundi vya uhalifu.
Amesema ujio wa jumuiya hiyo unakwenda sambamba na jitihada za jeshi la polisi katika kupambana na vitendo vya kihalifu na kukabiliana na Watoto wanao katisha masomo na kujiingiza katika vikundi viovu.
Kwa upande wake mwenyekit wa jumuiya hiyo Khalfani Ali Faki amesema lengo la jumuiya hiyo ni kuwasaidia vijana kusoma kwa bidii na kuwatoa katika vigenge hatarishi kama vile uhalifu na madawa ya kulevya hivyo ni muhimu kwa kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake ili lengo liweze kufikwa.
Amesema kwasasa kundi kubwa lililoharibika katika vikundi viovu ni vijana ambao wanategemewa kuwa ndio viongozi wa baadae hivyo ni vyema kuungana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha vijana hawapotei.
Akiwasilisha mada ya uwajibikaji katika uongozi mkufunzi Mohd Salim amesema kiongozi bora ni yule anaefuata maadili na kutochupa mipaka ya ungozi ili kujenga maelewano mazuri na anaowaongoza.
Nao washirki wa mafunzo hayo wameishukuru jumuiya hiyo kwa kuwapatia elimu hiyo na kuahid kuifanyia kazi ili lengo liweze kufikiwa kwa ufanisi Zaidi.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyowashirikisha wanachama na viongozi wa jumuiya ya EKWADEO yamefanyika katika ukumbi kilima ndege wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na jumla ya washiriki 136 wamepatiwa elimu hiyo.
MWISHO.
Comments
Post a Comment