WANAWAKE KISIWANI PEMBA WALILIA MILA ,DESTURI,MAVAZI YASIO RAFIKI KUENDELEA KUWA KIZINGITI USHIRIKI WA MICHEZO MBALI MBALI
Na,AMINA AHMED PEMBA .
BAADHI ya wanawake kisiwani Pemba Akiwemo Halima Juma Shehani,Pamoja na Zulfa Shaame Ali wote wakaazi wa Madungu wameeleza mitazamo yao juu ya kutokushiriki michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu , pamoja na mazoezi ya viungo katika viwanja mbali mbali vya michezo ambapo wamesema kuwa mila na desturi zao zinawawia ugumu kushiriki katika harakati hizo.
Wamesema mavazi yasio rafiki endapo yatavaliwa na wanawake ikiwemo suruali ni kuenda kinyume na mila silka pamoja na utamaduni wa jamii kisiwani humo .
Aidha wameeleza kuwa maadili ya jamii nyingi kisiwani Pemba yanakwenda sambamba na mfumo wa miongozo yq maisha dini waliyokulia hivyo suala hilo ni changamoto kwa upande wao.
Wamesema iwapo kutawekwa mavazi maalum ya kuvaliwa na wanawake watakaoamua kushiriki michezo ambayo yatazingatia staha na heshima ya mwanamke huenda ushiriki wao utaongezeka katika tasnia hiyo ya michezo.
Aidha wakatumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kutoa elimu juu ya suala hili ili iwezo kuwasaidia kuongeza ushirimi wao bila kuendana kinyume na mafundisho ya kidini.