WATU WENYE ULEMAVU WA AKILI PEMBA WAFUTARISHWA WAZIRI HARUSI ATUMA UJUMBE HUU KWA WANANCHI .

NA -AMINA AHMED MOHD ,PEMBA.
 WAZIRI  wa Nchi ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar  Harusi Said   Suleiman  amewataka wazazi  wakike na wakiume pamoja na wadau wa  kutetea haki za watu wenye ulemavu  kuongeza umakini  katika kusimamia malezi ya watoto na watu   wenye ulemavu wa akili  zaidi katika katika  kipindi kijacho cha msimu  wa  siku kuu ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Kauli hiyo ameitoa  leo  katika ukumbi wa Tibrinzi Chake Chake  mara baada ya kumaliza ghafla ya  Iftari  ya pamoja kati ya  watu weye ulemavu wa akili,wazee walezi  wasimamizi wadau na watetezi wa haki  za watu hao  iliyoandaliwa na Jumuia ya watu wenye Ulemavu wa Akili Zanzibar  upande wa Pemba  .

Amesema  jukumu la kuwatunza na kuwalinda watu wenye ulemavu wa akili  dhidi  ya vitendo  vya udhalilishaji linahitaji  umakini zaidi kwa vile wao ndio waathirika zaidi katika matendo hayo.

" Tunaelekea katika siku kuu nawaomba wazazi akina baba na akina mama tuwaangalie sana watu wetu hawa  tuweke jicho lenye uangalizi maalum huu sio wakati wa kuwaacha peke yao ".

" Tusije tukwaachia tu kama Mbuzi au Ngo'mbe waliokatwa kamba wakawa wanazurura  tu mitaani na tuhakikishe tunatoka nao na kurudi nao mkononi ili wasije wakapatwa na majanga haya yaliotawala duniani kote ya unyanyasaji  ambayo ni hatari zaidi kwa upande wao".

Waziri Harusi  pia  amewaasa  wananchi  kuendelea kuwatunza kuwajali kutetea haki zao pamoja na kuwathamini watu wenye ulemavu  kwa vile suala hilo linaweza kumfika mtu yeyote .


 Aidha  Waziri huyo ameipongeza jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili kwa upande wa Pemba kwa  kuwakutanisha watu wenye ulemavu wa akili   kutoka sehemu mbali mbali katika futari ya pamoja ambapo ameziasa jumuia nyengine kuiga  suala hilo .

Hata hivyo  waziri huyo amewaasa waumini wa dini  ya kiislam   Zanzibar   kuendeleza  matendo mazuri wanayoyafanya katika mwezi mtukufu wa ramadhan  ikiwemo kusoma qur -an ,mashirikiano  kusaidiana na  pamoja na kumuamudu mwenyezimungu katika miezi mengine ili kupata ujira zaidi  .

Kwa Upande wake Mkubwa Ahmed Omar ambae ni Mjumbe wa kamati tendaji wa jumuia hiyo Zanzibar amesema kuwa jumuia hiyo  itaendelea kutetea haki za  watu  wenye ulemavu  wa akili pamoja na kuzisimamia ipasavyo kwa maslahi na  maendeleo ya watu hao.

Akizungumza  katika ghafla ya iftari hiyo  mlezi wa jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili  kwa upande wa Pemba  Sheh Said Ahmad Muhamed amesema suala hilo liliofanywa  na jumuia hiyo  ni miongoni mwa mambo yaliyohimizwa katika Uislam  ni pamoja na  kuwatendea wema   watu wenye mahitaji maalum  ambapo amewaasa waislam wote kuendelea kuwatendea weka watu hao.

Akitoa neno la shukurani kwa wanajumuia hiyo Afisa mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Zuhura Mgeni Othman ameishukuru jumuia hiyo  kwa kuandaa ifatari hiyo ambapo amesema kuwa   wadau wa kutetea  haki  za watu wenye uleamavu wataendelea kushirikiana vyema na jumuia hiyo katika kuona  wanshiriki ipasavyo katika  fursa mbali mbali .

Jumla ya watu wenye ulemavu wa akili 90,wazazi walezi wasimamizi wa watu hao pamoja  wadau  kutoka maeneo mbali mbali kisiwani humo wameshiriki katika iftari hiyo maalum iliyoandaliwa na Jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili ofisi ya Pemba kwa kushirikiana na ofisi ya  Makamu wa kwanza wa rais  na wadau wengine mbali mbali.


 mwisho

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.