WANAWAKE MUSIOGOPE KWENDA MAJIMBONI UCHAGUZI WA 2025
NA ASIA MWALIM.
WAKATI wigo wa demokrasia na utawala bora unatunilwa nchini juhudi za kupunguza pengo kati ya wanawake na wanaume katika uongozi zinaendelea kupata mafanikio.
Uamuzi wa Tanzania wa kuridhia mikataba ya kikanda na Kimataifa inayosisitiza usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume katika uongozi na ngazi za maamuzi umeziongeza chapuo juhudi hizi.
Tafauti na zamani, wanawake wa Zanzibar hivi sasa wanathubutu kugombea na kushinda katika nafasi mbaali mbali za uongozi, zikiwemo za udiwani, uwakilishi na ubunge, lakini bado kiwango hakiridhishi.
Vyama vya siasa vinategemewa kuwa njia kuu ya kuingia katika kinyanganyiro cha uchaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 39 (1) (C) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), ambayo inamtaka kila anae wania uongozi anapswa kupendekezwa na chama cha siasa.
Hapa inafaa kukumbushana kwamba hapa kwetu hapana mfumo wa kuwa na wagombea hurya, yaani asiyetumia chama cha siasa kuingia katika uchaguzi.
Ujio wa mfumo vyama vya vingi vya siasaTanzania umetoa fursa sawa kwa wananchi wengi, wakiwemo wanawake, kugombea nafasi za uongozi.
Mwanaasha Khamis Juma, Mwakilishi wa Jimbo la Dimani kupitia tiketi ya Cha Cha Mapinduzi (CCM)ni miongoni mwa mwanamke anaetumikia nafasi hiyo kwa awamu mbili, baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu unaofanyika kila baada ya miaka 5.
Mwanamke huyo amekua mfano wa kuigwa na wanawake wengine wa Zanzibar kwa harakati zake za kuhakikisha anaendelea kuongoza nafasi hiyo bila ya kubabaishwa na wale wanaoona mwanamke hafai kuongoza kwa vile dhana za mfumo dume inawatala.
Huyu ni mwanamke anayejutuma kuwapatia watu waliomchagua maendeleoa na juhudi zake zinawazidi baadhi ya wanaume wanaoshka nafasi ya uongozi kama yak wake.
"Hatua ya mwanamke kuongoza nafasi ya uwakilishi sio jambo dogo, kitu cha msingi ni utayari na kujikubalisha kwa jamii unayoiongoza. Watu hawachagui jinsia bali ni namna gani utaweza kuongoza na kuwatumikia" alisema.
Akizungumzia uchaguzi wa ccm uliofanyika mwaka jana, Mwakilishi huyo alisema kwa sasa hali inatia moyo kwani wanawake wengi waligombea nafasi mbali mbali za uongozi na kushinda licha ya kwamba bado mfumo dume unatokota, lakini sio kwa kasi kama ile ya miaka ya nyuma.
Alisema Safu ya uongozi kwa wanawake kupitia CCM na katika serikali inaendelea kukua, lakini kwa bahati mbaya idadi imeongezeka kywa kupitia nafasi wanazopata za uteuzi na sio kuchaguliwa majimboni.
Idadi ya wanawake waliotoka katika majimbo katika Baraza la Wawakilishi imeongezeka kwenye kutoka saba mwaka 2015 hadi wanane mwaka 2020.
Katika mwaka 2020, wanaume waliojitokeza kugombea uwakilishi ni190 na walioshinda 42, ambapo wanawake waliogombea ni 61 na wanane walishinda.
Kati ya wajumbe wanawake 29, wajumbe 8 ni kutoka katika majimbo na 21 wameingia kupitia viti maalumu na kwamba hadi kufikia Januari mwaka 2024, Zanzibar ina mawaziri wanawake 6 na maniabu waziri wanawake watatu katika wizara 18.
Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, wanawake tujitokeze kugombea katika majimbo ya uchaguzi ili tuongeze idadi katika vyombo vya kutunga sheria.
Huu ni wakati wa kujitokeza wanawake kuwania nafasi za uongozi kutokana na jamii kubadilika na kuona juhudi zinazochukuliwa na wanawake waliopata nafasi waliopata nafasi ya kuongoza kwenye majimbo ya uchaguzi.
Akitolea mfamo uliotokea mwaka 2015_2020 alisema alikua Mwakilishi wa Jimbo la Chukwani wa kuchaguliwa na wananchi na kuongoza miaka mitano, wakati akijipanga kugombea tena tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ilikua katika marekebisho ya mgawanyo wa majimbo na kulifuta jimbo hilo kuwa jimbo la Kiembesamaki.
Hali hiyo ilimpa mashaka kidoho kwani jimbo alilolizoea kuongoza kwa miaka itano limefutwa hatimae kutafuta jimbo jipya kuanza upya haraki za siasa.
Mabadiliko hayo yalibabaisha kidogo lakini hakukata tamaa aliqmua kujitosa kwa mara nyengine katika jimbo jipya la Dimani, Mkoa wa mjini Magharibi kwa nafasi ile ile ya uwakilishi na kupambana na wagombea wsiopungua 11 wakiume hatimae kuibuka tena na ushindi.
"Kiongozi yoyote anapo fanya vizuri, kwa wale waliomchagua ana matumaini makubwa ya kurudi tena kwenye nafasi hiyo na mara nyengine hupewa zaidi ya hiyo" alisema.
Aliwataka wanawake kuacha woga na kujitokeza kuwania katika majimbo ya uchaguzi ili kufikia usawa kwenye nafasi za uongozi na maamuzi ndani ya vyombo vya kutolea maamuzi na kutunga sheria.
Tokea nchi za Afrika ya Mashariki zipate uhuru na Mapinduzi kwa Zanzibar katika miaka ya 1960 wamekuwepo viongozi wakuu wa nchi zaidi ya 30 na wote walikuwa wanaume mpaka mwezi Machi, 2021 pale Mama Samia aliposhika usukani wa kuiongoza Tanzania.
Tukio la Mama Samia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewapa hamasa wanawake nchini ambao wanazo sifa za uongozi kujitokeza mbele kuwania uongozi ili na wao kama wenzao wanaume wachangie maendeleo na mafanikio ya nchini yao.
Ongezeko la wanawake katika nafasi za uongozi ni utekelezaji wa vitendo dhamira kuweka usawa katika uongozi kati ya wanawake na wanaume na kuondoa fikra na dhana potovu ya kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi Mkuu wa Tanzania.
Aliongeza kuwa Uongozi wa Mama Samia sio tu umethibitisha kwamba mwanamke anaweza kuiongoza Tanzania, bali umeweka ushuhuda wa hilo kufanyika kwa mafanikio na uadilifu.
“Dk. Mwinyi kwa kutambua umuhimu wa wanawake na kuwaamini kwenye uongozi, amewapa nafasi mbali mbali na muhimu kwenye ngazi za maamuzi, ni jambo muhimu sana”, alisema Mwanaasha.
Sambamba na hayo aliwashauri wanawake kuendelea kujitoa zaidi katika nafasi mbali mbali, ili kufikia usawa wenye hadhi sawa katika nafasi za kugombea uongozi kati ya wanawake na wanaume hasa majimboni.
Zanzibar ina majimbo 50 ya uchaguzi, Mkoa wenye majimbo mengi ni Mkoa wa Mjini Magharibi (19) na Mkoa wenye majimbo machache ni Kusini Unguja (5)
Aidha idadi ya wadi zinatofautiana kwa Mikoa, Mkoa wenye Idadi kubwa ya wadi ni Mkoa wa mjini Magharibi (44), ikifuatiwa na Mkoa wa Kusini Pemba wadi (19), Mkoa wenye wadi chache ni Kusini Unguja wadi (12).
WANAWAKE WANAOTAKA UONGOZI
Baadhi ya wanawake wanaotaka nafasi za majimboni kupitia vyama mbali mbali vya siasa Zanzibar walisema, mwanamke huyo ni mfano wa kuigwa na wanawake wengine, hivyo watajitokeza kwenye majimbo ya uchaguzi wakati ukifika.
WANANCHI WALIOMCHAGUA.
Baadhi ya wananchi wa jimbo la Dimani, Hassan Said Ussi na Abdillah Mussa Hamad walisema, kutokana na huruma za kiongozi huyo, hawaoni haja ya kubadilisha kiongozi mwengine .
"Bado tumejenga matumaini kwa mwanamke huyu, tunatamani kupata viongozi wanawake kwenye nafasi nyengine ndani ya jimbo letu" walisema.
Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar, Dk Mzuri Issa Ali, alisema umefika wakati kuondoa vikwazo vinavyokwamisha usawa kwa wanawake na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kuweka sheria rafiki zitakazotoa muongozo wa nafasi za uongozi na sio kugawa nafasi za uteuzi kama zawadi.
Alisema kutokana na hali ilivyo katika vyama vya siasa ipo haja ya vyama kulazimishwa kuwa na usawa wa 50 kwa 50 kwenye vyombo vyao vyote vya maamuzi ili wanawake wapate nafasi za majimbo.
"Bado vyama vya siasa havijazingatia usawa, kuanzia kwenye sheria, uchaguzi wa ndani ya vyama na majimboni, mbali ya kupokelewa vizuri na sio kwa uadui" aliongeza.
Alisema TAMWA, kwa kushirikiana na wadau wengine, kama Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na PEGAO ) imekua ikitoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake ili kuhakikisha wanapata haki sawa katika nafasi za uongozi wa kuchaguliwa na kujitokeza kwa wingi kipindi kitapofika.
KATIBA YA ZANZIBAR
Katiba ya Zanzibar ya1984 inaeleza katika kifungu 21(2) kuwa kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu na yanayohusu taifa lake.
Aidha katiba hiyo katika marekebisho ya 2010 imeeleza katika kifungu nambari 67 (1) kuwa kutakuwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wanawake kwa angalau asilimia 40 ya wajumbe wote wa kuchaguliwa katika majimbo.
DIRA YA ZANZIBAR 2050
Dira ya Zanzibar katika maazimio ya 2.5.1 hadi 2.5.9 yameeleza masuala ya usawa wa jinsia na kuondoa unyanyasaji wa kijinsia na kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wanawake ikiwemo kuinua na kutoa nafasi za uongozi kwa wanawake katika jamii.
Vile vile inazungumziwa kuongeza fursa na kuwawezesha wanawake katika vyombo vya kutolea maamuzi na kwenye shughuli za uchumi, kijamii, siasa katika ngazi zote za utawala na huduma za sheria.
SERA YA JINSIA YA ZANZIBAR
Sera ya jinsia inaelezea ushiriki wa wanawake katika vyombo vya utoaji wa maamuzi katika ngazi zote ni mdogo. Kwahivyo, serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, itafanya juhudi kuona kuwa makundi yote na yaliyopembezoni wanapata fursa hiyo.
ITIFAKI YA SADC
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) inaeleza katika mkataba uliotiwa saini mwaka 2008 umuhimu wa kuondoa utafauti na kutowatenga wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kuwasaidia katika usawa wa kijinsia.
mwisho
Comments
Post a Comment