TAMWA YAPONGEZWA KUTOA MAFUNZO YA UONGOZI KWA WANAWAKE
.
WANAWAKE wa rika tofauti wamepongeza juhudi zinazochukiliwa na asasi za kiraia ikiwemo TAMWA katika kuwajengea uwezo katika mambo yanayowahusu ili kufikia azma ya kuwa viongozi.
Walitoa pongezi hizo wakati wakizungimza na muandishi wa habari hizi kwenye maeneo mbali mbali ya Zanzibar .
Zainab Saleh Salum, maarufu kama ZASASA, alisema, kupitia mafunzo yanayotolewa na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania- Zanzibar, wamepata uzoefu wa kujieleza na kutoa maoni yao kwa jamii bila woga
Aidha walisema, kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kila mtu akiwa mwanamke au mwanamme hivyo hawatosita kujitokeza siku zitakapo wadia.
Maryam Saleh Ali, (44) Diwani wa viti maalumu wilaya ya Magharibi B, alisema kupitia vyombo vya habari mbali mbali amerlimika kuhusiana na elimu ya uongozi kwa wanawake jambo ambalo linawahamasisha zaidi.
Ashura Khamis Mwadini,(28) Radhia Abdallah (28) waliomba taasisi nyengine kutilia mkazo suala la wanawake na uongozi kwa kutoa mafunzo zaidi ili kutoa hamasa zaidi hasa kwa vijana jambo ambalo litabadilisha fikra na mitazamo wa jamii.
Mratibu wa Mradi wa kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Maryam Amer Chum, alisema mara kadhaa wamefanya mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya uongozi kilichobaki ni wao wenyewe kujitoa wakati utakapofika.
Alisema muda wa kuyatumia mafunzo hayo kwa vitendo umefika hakuna haja ya kurudi nyuma linapokuja suala la kudai haki zao za kikatiba na kisheria ili kufikia lengo la usawa kwa wanawake na wanaume katika uongozi wa nafasi mbali mbali.
Comments
Post a Comment