NAIBU WAZIRI AWAFARIJI AKINA MAMA HOSPITALI NA KUUNGA MKONO SERIKALI KUDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO.

Na AMINA AHMED MOH'D


NAIBU  Waziri wizara ya maji nishati na madini  Zawadi Amour Nassor ambae  pia ni mwakilishi wa Jimbo la Konde amesema kuwa kukabidhi misaada ya vifaa mbali mbali ikiwemo sabuni,nguo za watoto pamoja na fedha kwa mama waliojifungua ni katika kuidaidia serikali kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Amesema  jitihada zilizochukuliwa na raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Hussein Ali mwinyi za kujenga mahospitali yenye vifaa mbali mbali iliwemo incubater zimepunguza Kwa kiasi kikubwa vifo vya watoto njiti kisiwani Pemba.

 Zawadi ameyasema hayo katika ziara yake alioambatana na jumuiya ya wanawake Jimbo la konde UWT ya kutembelea pamoja na kuwafiriji akina mama na watoto  wanaoendela na matibabu  katika mahospitali .

Amesema Hatua hio umekuja kupunguza vilio Kwa akina mama  hivyo wananchi kuendelea kumpongeza pamoja na kumuombea dua ili aendelee kutekeleza yale alioyaahidi pamoja kutekeleza ilani ya chama Cha mapinduzi ccm.

Aidha amesema kuwa awali  ilikua hakuna kifaa hivyo hali ambayo ilipelekea vifo vingi Kwa watoto njiti lakini kutokana na jitihada zake watoto wanaozaliwa kabla ya Mda wamekua wakipata huduma na kuwanusuru na vifo .

Akizungumza na madaktari wakunga  katika hospitali ya kinyasini amewanasihi mara baada ya kuwapatia huduma ya kujifungua kuwapa elimu wazazi ili kuwaepusha na vifo vya mara Kwa mara ambavyo hutokea mara baada mama kurudi nyumbani .

Katika ziara hio pia tulipata kuzungumza na dk dhamana wa hospitali ya kinyasini dk Ramadhan Faki Ali na kusema kuwa kitendo alichokifanya mwakilishi wa Jimbo la konde ni chakuigwa hivyo kuwaomba na wengine kuiga mfano huo ili kuwafiriji wazazi waliopo hospitalini.


Hata hivyo Dk Saidi kutoka spitali ya micheweni ametoa shukrani kwa mwakilishi Kwa kuwatembelea akina mama hao na kuwafiriji na kumtaka kuendeleza moyo  wa kujitoa Kwa wengine siku hadi siku.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.