NAIBU WAZIRI AGUSWA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

 WANANCHI wenye mahitaji m, pamoja na wazee wameiomba serekali ya mapinduzi ya Zanzibar kuwaona pamoja na kuwafiriji ili kuondokana na hali duni  walizonazo .NA AMINA AHMED MOH'D PEMBA.

Wameyasema hayo mara baada ya kutembelewa na naibu Waziri wizara ya maji nishati na madini Zawadi Amour Nassor ikiwa ni katika ziara yake ya kuwatembelea na kuwafiriji wananchi hao .

Wamesema kuwa viongozi hawaoneshi kuwajali mara baada ya Kufikiwa na matatizo mbali mbali hivyo kuimba serekali kuwakumbuka ili kupata faraja .

Katika hatua nyengine wameiomba serekali kulichukulia hatua suala la kesi za udhalilishaji ili kupunguza matendo hayo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika Kwa ziara hio  Zawadi Amour Nassor amesema lengo la ziara hio ni kuwatembelea wananchi wanaokabiliwa na changamoto mbali mbali   pamoja na kuwafiriji ili kupata faraja katika nyoyo zao .

 Mwanakombo Omar Ali kutoka konde amesema ni vyema serekali kuwaangalia watu wenye mahitaji maalum Kwa upeekee ili waweze kunufaika na serekali Yao .

Comments

Popular posts from this blog

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

UHABA WA VITUO VYA POLISI WILAYA YA CHAKE CHAKE BADO MLIMA MREFU KUDHIBITI UHALIFU VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAMU.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.