MWANAMKE ANAESIMAMIA WATOTO WA KIKE VIJIJI KUPATA HEDHI SALAMA NA KUIMARISHA AFYA YA UZAZI



NA ASIA MWALIM 

WADAU wa Elimu wanakadiria kuwa katika siku za masomo kwa mwaka siku 36 hadi siku 60 wasichana huwa katika siku za hedhi ambapo asilimia 58 kati yao wana uwezekano mkubwa wa kukosa masomo kutokana na kushindwa kununua vifaa.

Wasichana wanaofikia umri wa kupevuka kimaumbile wanakutana na vikwazo vya usawa katika upatikanaji wa elimu na fursa za maendeleo yao ikiwemo nafasi za uongozi hasa wanapofika umri wa kuanza hedhi.

Hedhi si jambo linalozungumzwa kwa uwazi katika jamii zetu kwa kua limefungamanishwa na aibu, hali hiyo huwafanya wasichana kukosa msaada unaohitajika na mara nyengine kukosa haki zao.

Kushindwa kufahamu hedhi salama, kukosa uwezo wa kununua vifaa vya hedhi na mazingira yasiyorafiki vijijini ni miongoni mwa vikwazo ambavyo kwa watoto wa kike kufikia uongozi.

Miaka iliyopita jamii yetu ilishindwa kutilia maanani sana afya ya uzazi kwa wasichana, kukosa taarifa sahihi ya afya zao hasa wakati wa hedhi kumepelekea kujitokeza watu kuongoza jambo hilo ili kufanya marekebisho yanayohitajika.

Miongoni mwa wanawake waliojitokeza mstari wa mbele kuongoza juhudi za kutunza hedhi salama kwa wasichana mashuleni ni Brenda Geofrey Ndossi (31) ambae ni Mkurugenzi Miradi kituo cha Barefoot College International, kilichopo Kinyasini Zanzibar.

Kabla ya kuanza shughuli hiyo, alionesha nguvu yake kama mwanamke kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii  kuanzia mwaka 2019 mpaka 2022 akiwa kituoni hapo.

Alibaini kuwa wazazi wengi wanaogopa kutoa elimu hiyo wakidhani kuwa wasichana watakuwa na tabia mbaya lakini sio kweli, msichana kuwa na uelewa kuhusu mwili wake Pamoja na kazi ya kila kiungo ni vizuri.

Kwa vile amekusudia kufanya programu za kuwanyanyua wanawake, kwa miaka mingi amekuwa akitoa elimu za stadi za maisha kwa wanawake mbalimbali, kwa mfano kushirikiana na taasisi nyingine kuwasaidia wasichana waliopata mimba kwenye umri mdogo kwa kuwapa mafunzo ya amali ambayo yatawasaidia kupata kipato cha kulea watoto wao.

Mbali na shughuli hiyo,amefanikiwa  kusaidia wasichana na wanawake kujiinua kiuchumi kupitia miradi ya ufugaji nyuki, ushonaji na mafunzo ya umeme wa jua.

Idadi ya wasichana waliopatiwa taula za kike tangu kuanza mradi huo ni zaidi ya wanafunzi 3200 kutoka shule mbalimbali katika ksiwa cha Unguja na Pemba.
 
"Kupitia jamii inayonizunguka, kwa ukubwa kabisa mtu anaenipa msukumo ni kumuangalia rais wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ambaye ni rais wa kwanza mwanamke nchini ambae ametokea katika nafasi za chini za uongozi mpaka sasa kuwa kiongozi mkubwa wa nchi" alisema.

Brenda alisema Mtu mkubwa anaemuiga katika utendaji wake ni Dk. Samia Suluhu Hassan, alisema mtu hahitaji nguvu nyingi kuona jinsi Mama Samia anavyofanya kazi ya kufungua milango ya nchi lakini pia mara nyingi kuonesha moyo wa kipekee katika kusaidia watu kwa nyakati tofauti. 

Aliongeza kuwa tofauti na mheshimiwa Rais mama yake mzazi ambae ni mwalimu wa wengi, ameweza kuwa na mchango mkubwa wa kumkuza na kumsaidia kuwa na ujuzi tofauti tofauti ambao unamuongoza vizuri katika nafasi yake ya uongozi.
 
Kitu kikubwa kilichompa msukumo kufanya shughuli za kuwasaidia watoto wakike kupata hedhi salama ni baada ya kubaini wasichana wengi kutoka kaya za vijijini hawana taarifa sahihi kuhusu afya zao lakini pia kuwa na taarifa nyingi ambazo sio za ukweli kuhusu afya zao. 

" Kwa kuona tatizo la , kituo chetu kupitia mradi wetu wa taulo za kike tumeamua kutoa elimu kwa kushirikiana na watu kitengo cha afya" alisema. 

Mbali na ugawaji wa taulo za kike, pia hutoa sabuni na nguo za ndani kwa wanafunzi mashuleni na wasichana mbalimbali zaidi kwa kaya na shule za vijijini.
 
Alitaja tabia zilizochangia mafanikio  katika shughuli ya kuwasaidia watoto wa kike alisema anapenda kuwasaidia watoto wa kike zaidi wanaotoka vijijini na waliokosa haki ya elimu kutokana na sababu mbali mbali.
 
"Kwanza kabisa ni msukumo uliopo ndani yangu na dhamira yangu ya siku nyingi katika kusaidia wasichana na wanawake sana sana wanaotoka katika jamii za vijijini na ambao hawajapata nafasi kabisa ya kupata elimu" alisema.
 
Kuhusu malezi yake alisema wazazi wake walimlea katika mazingira yaliyomjenga kuwa kiongozi kuanzia kwenye ngazi ya familia mpaka kwenye jamii. 

Aliongeza kuwa Uongozi mzuri unaanza katika ngazi ya familia lakini pia kujiweka katika nafasi ya mtu mwingine, kuwa na huruma na moyo wa kusaidia wengine wenye uhitaji.

Miongoni mwa mambo yatakayo Acha alama na kumbukumbu nzuri katika uongozi wake ni kusimamia elimu wanazotoa zisiishie tu kwa wanawake bali ziende mbele na kugusa jinsia ya kiume.

Hivyo wamekuja na mpango mkakati wa kuwafundisha wanaume ufugaji nyuki ili waweze kusaidia wanawake kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo uwekaji wa mizinga kwenye miti pia kukaa na wanafunzi wa kiume kuwaelimisha kuhusu balehe na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko katika miili yao wakati wa balehe.

Malengo yake ni kuhakikisha siku moja wasichana wote Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wana taarifa sahihi zinazohusu hedhi salama na pia wana access ya taulo za kike na nguo za ndani kila wanapohitaji.
 
Jamii tunayofanya nayo kazi inatoa mashirikiano ya kutosha na tupende sana kuwashukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi ambao tuna mashirikiano nao katika kufikia wananchi wengi zaidi na kuwawezesha katika nyanja zote.

Alieleza siri kubwa ya mafanikio hadi kufika hatua hiyo ni kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mungu katika kazi zake zote anazofanya.

Aliwasihi wazazi na walezi kuwapa elimu Watoto wa kike katika maswala yanayowahusu kabla ya kukutana nayo, mfano suala la hedhi na namna ya kujikinga na mimba za utotoni. 

"ni muhimu mtoto wa kike kujua kuhusu hedhi kwamba ni kitendo cha kibailojia ni kawaida kwa mwili wa mwanamke kujisafisha kila mwezi, elimu kuhusu mimba za utotoni, itasaidia kuzikinga na hazitakuwepo" alisema.

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ni mfano bora kwa watoto wa kike, kupitia yeye tunaona mwanamke anaweza kushika nafasi za juu kabisa za uongozi na kufanya vizuri kabisa.
 
vijana, kutenga muda kujifunza kitu kipya kila siku, kwani elimu ndio mkombozi wa mambo mengi sana kwa dunia ya sasa kwa kupata uhusiano uliopo kati ya hedhi na mfumo wa uzazi wa mwanamke ikiwa ni pamoja na kuhusisha viungo vinavyohusika.

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana Mpaka sasa wanafunzi wameweza kujitambua, kujua hedhi inavyotokea na kuwa mawakala wa wasichana wengine katika kaya zao kwa kuwaeleimisha walichojifunza.
 
Anaepewa kilima hakoseshwi mwendo na hapa anaeleza changamoto zinazojitokeza katika harakati zake ni gharama kubwa ya vitambaa vya kutengeneza taulo za kike, taulo za kufua (reusable) ambazo mahitaji yake ni vitambaa aina tatu ambavyo vyote vinauzwa nje ya nchi na kwa gharama kubwa sana.

Pia Gharama katika kulipa wasichana ambao ni washonaji wa taulo hizo, pamoja na gharama za umeme.
 
Aliishauri jamii na wazazi, kuachana na imani potofu kuhusu uvaaji wa pedi kwani ni kikwazo kinachojitokeza zaidi maeneo ya vijijini.
 
Kazi hiyo anaifanya kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali kupitia kituoni cha Barefoot College International Zanzibar katika kutoa taula za kike, ikiwemo Frey Charitable Foundation, Basque Agency, Dnata, na wengine.
 
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa skuli ya kijini, Bahati Faki Omar, alisema wamefurahishwa kupatiwa taula za kike kwa ajili ya hifadhi, awali walitumia vitambaa vya kawaida.

Mratibu Afya ya mama na mtoto wilaya ya Magharibi B, Safia Khamis Juma, alisema mbali na kuvaa taula za kike kwa njia sahihi pia aliwasisitiza wanawake kula vyakula aina ya mboga za majani na matunda ili kuimarisha afya zao kwani wanapoteza madini ya chuma kila mwezi.

Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uchumi na Uwezeshaji, masuala ya kazi na Uwezeshaji Zanzibar, Maryam Juma Abdallah, alisema bila ya wanawakwe kuwa na afya nzuri, hawawezi kujenga uchumi imara wa nchi, wala kuwa kiongozi.

Wanawake ni viongozi na walezi wa familia wanapaswa kutunza na kuimarisha afya zao kwa lengo la  kufikia maendeleo yao na taifa kiujumla.

Zanzibar kama zilivyo nchi nyengine duniani inasherehekea siku ya wanawakwe, kutokana na umuhimu wake wa kumuwezesha mwanamke kupiga hatua muhimu za kimaisha na kukumbusha jamii juu ya haki za wanawake.

Hatua ya kugawa vifaa na kutoa elimu ya afya skulini hapo, ita wawezesha wanafunzi wakike kushiriki vizuri masomo yao bila ya kusumbuliwa na tatizo la kiafya na saikolojia.

Aliwapongeza Barefoot kutoa elimu ya uzazi, hedhi salama kwa lengo la kuepusha tatizo la mimba za utotoni, magonjwa ya zinaa na kujitambua pia aliwataka wanafunzi wakike kutumia vizuri vifaa na elimu waliopatiwa ili kuwa na afya bora, kuwapatia elimu hiyo wanawake wengine ili kufikia ndoto zao.

Sambamba na hayo aliwasisitiza wanafunzi kuwa majasiri na kujikita katika masomo na kupinga udhalilishaji wa kijinsia ili kufikia ndoto zao za kuwa viongozi bora.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.