WANAWAKE WAASWA KUGOMBEA MAJIMBONI BILA WOGA 2025 ,NA KUACHA KUSUBIRI NAFASI ZA KUTEULIWA.

NA AMINA AHMED, PEMBA. 


KUFUATIA kutokuwepo kwa Usawa wa kijinsia katika vyombo vya kutolea maamuzi Wanawake wameaswa kugombea nafasi za uongozi wa majimbo katika uchaguzi  mkuu 2025  bila kuogopa vitisho vinavyotolewa na  watu wachache na wasiopenda kuona wanafika mbali katika maendeleo na kuishia katika nafasi za kuteuliwa kila siku. 

Kauli hiyo ya kuwahamasisha imetolewa  na aliewahi kuwa Mbunge wa  Chonga Chake Chake Leila Nassor Khamis alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa habari hizi maalum za uongozi kwa wanawake aliefika nyumbani kwake Chanjaani. 

Alisema iwapo watafanya maamuzi juu ya jambo hili kutasaidia kufikia usawa wa kijinsia katika vyombo vya maamuzi ambao bado haujafikiwa kutokana na waliowengi kuziogopa nafasi za majimboni  ambazo zina fursa zaidi. 

Aidha aliwataka wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali zitakapotangazwa ikiwemo nafasi ya ubunge  uwakilishi na udiwani katika majimbo  na kuacha kuwaachia wanaume peke yao kuitumia fursa hiyo kwa kuogopa vitisho. 

" Jimboni hakuna kikubwa kinachitufanya wanawake tushindwe kuongoza sheria ndio zile zile kanuni ndio zile zile  siku zote, kufanya jambo kwa maslahi ya unaowaongoza  bila ya upendeleo au ubaguzi wa aina yeyote  tuzifuate fursa za majimboni tunaziweza, tusisubiri za kuteuliwa kila siku. 

" Wanawake wenyewe ndio ambao tutaweza kuzisemea haki zetu  na ni kwa kiasi gani tunaweza kuzitetea  ni kugombea  kwa wingi kupitia nafasi za majimboni ili tuweze kufika katika vyombo vyakutolea maamuzi. 

" Changamoto ni za kawaida ,  tunatakiwa tujiamini  na kujua tunachotakiwa kukifanya inatosha wewe kuingia jimboni tuzichangamkie fursa hususan ni wanawake vijana". 

" Hakuna chochote kibaya  endapo mwanamke atakuwa kiongozi kuombwa rushwa au kuwa na tabia mbaya ni mtu mwenyewe tu  na endapo hautokuwa tayari kufanya hivyo wala hakuna atakaekulazimisha."Alisma bi Leila Aliwahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi ikiwa ni pamoja na  Ubunge wa jimbo Chonga Wilaya ya Chake Chake. 

Hadi kumalizika uchaguzi mkuu  mwaka 20220 Idadi ya wabunge wanawake 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.