MAFUNZO MAALUMU JUU YA MATAYARISHO YA KUSTAAFU KWA WATUMISHI WA UMMA YATOLEWA NA ZSSF KWA KUSHIRIKINA NA TCB BANK.

NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA. 

WATUMISHI wa umma  wanaotarajiwa  kustaafu  kisiwani Pemba  wameaswa  kujiwekea malengo ambayo yatawasaidia kuendeleza vyema maisha yao na kuwaondoshea usumbufu  unaowapata wastaafu wengi  mara baada ya kumaliza muda wa utumishi  na kurudi katika jamii.

 Ushauri huo umetolewa na Afisa mdhamini Wizara ya Nchi ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, utumishi na utawala bora Halima Khamis Ali   Alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa watumishi wanaitarajiwa kustaafu  juu ya maandalizi ya kustaafu  yaliofanyika katika ukumbi wa  ZSSF Tibirinzi Chake Chake .
 Amesema iwapo maandalizi ya mapema katika kuyakabili maisha baada ya utumishi   yatafanyika changamoto za maisha afya  ugonjwa na mengineyo  ambazo zinawakabili wastaafu wengi wanaomaliza muda wa utumishi maisha bila ya utumishi yatakuwa ya   kawaida yenye utaratibu unaoendana na jamii  .

 Akizungumza na watumishi hao wanaotarajiwa kustaafu Mkurugenzi wa Zssf Pemba Said Maalim Said amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwasadia watumishi wa umma kuwa na uelewa juu ya matumizi sahihi ya hakiba zao walizoweka  katika Mifuko ya hakiba  mbali mbali ikiwemo zssf  na kuweza kuendesha maisha yao  watakapomaliza utumishi. 

 Kwa upande wake Meneja  wa TCB tawi la Pemba Shomari Mrisho  Amewaasa watumishi hao wanaotarajiwa kustaafu  kuitumia benk hiyo  katika kuendeleza vipaji vyao na fursa walizokuwa wameziwacha kutokana na kutumikia Taifa  ikiwemo kufanya  Biashara. 
 Nao baadhi ya watumishi hao wanaotarajiwa kustaafu  wameishukuru Zssf pamoja na benk hiyo  kwa kuwapa mafunzo hayo ya kujiandaa  ambapo wamesema kutawasaidia   kuondokana na changamoto na kujua namna ya kuzitumia hakiba zao katika kuendeleza maisha yao ya kila siku. 

 Mafunzo hayo ya siku Moja kwa watumishi wanaotarajiwa kustaafu yamekusanya watumishi kutoka taasisi za serikali mashirika pamoja na taasisi za umma ambapo mada  juu ya matayarisho baada ya kustaafu, Namna ya kutumia hakiba na nywngizo zimewasilishwa kutoka kwa wakufuzi  kutoka chuo cha Uhasibu Tanzania TIRA, Pamoja na Bank ya TCB.


Mwisho 



Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.