KIJANA MWENYE ULEMAVU WA AKILI NA VIUNGO ALAZIMIKA KULALA CHINI YA KIVULI CHA MTI BAADA YA KUKOSA SEHEMU RASMI RASMI KWA ZAIDI YA MIAKA 2 SASA,AOMBA MSAADA KUONDOKANA NA KADHIA HIYO.
NA AMINA AHMED, PEMBA.
Nyuma ya Picha ya Kijana Omar Said Ali kuna mti aina ya mdimu pamoja na sofa ambalo limeharibika , Huenda usiamini lakini hilo sofa na hilo eneo chini ya mti wa mdimu ndio kitanda anacholazimika kulala kijana huyo mwenye ulemavu wa akili pamoja na baadhi ya viungo nyakati zote za usiku, ni kutokana na kukosa sehemu rasmi ya kulala huku ulemavu wake ukidaiwa kuwa ndio chanzo kikuu cha kupata madhila hayo.
Kijana huyo anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 38 mkaazi wa Vikunguni Chake Chake Pemba anaendelea kupata madhila hayo kwa zaidi ya miaka miwili sasa, ambapo kabla ya hapo alilazimika kulala mabondeni ambako alijenga banda la miti lakini watu aliodai kuwa ni wezi waliliharibu banda lake na kuiba bati zilizokuwa zimeezekw katika banda hilo na kushindwa kupata fedha kwajili ya kununua bati nyengine.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi kwa masikitiko na unyonge kijana omar alisema kuwa bado baadhi ya watu katika jamii na familia licha kuendelea kufanya shughuli mbali mbali inaendelea kumtenga kutokana na ulemavu wake .
Ambapo alisema kuwa "Naonakena kama mimi sio binaadamu ambae nimeumbwa kama wao, sishirikishwi, naonekana siwezi kutoa msaada wowote, nikifanya shughuli zangu za kimaendeleo baadhinya watu wananiharibia, nyumbani kwetu siingii isipokuwa kwa kuchukua chakula, kulala sisubutu kwa sababu niliambiwa mimi ndio chanzo cha kuingiza wadudu aina ya kunguni ".
Nilipigwa marufuku na baba yangu wa kambo nisilale kwa sababu nitaingiza kunguni, nikaamua kuhamia mabondeni ambako nafanya shughuli zangu za kilimo cha miche aina ya mivinje nilijenga banda lakini liliibiwa bati, mama yangu na watu wengi wanajua hilo lakini wanaona ni jambo la kawaida "
Omar anasema msaada wake mkubwa kwa sasa ni Mwenyezimungu pekee ambae amemjaalia kumpa mtihani huo, huku watu wachavhe wenye moyo wa kumsadia kwa pale wanapoweza wakiendelea kumuunga mkono ikiwemo jumuia ya ya watu wenye ulemavu wa akili.
"Bado tunaonekana sisi ni watu wa kuonewa kuzushiwa maovu na kutengwa, kutokushirikishwa imefikia pahali makosa makubwa ya kufanya udhalilishaji tunazushiwa, wanafanya watu wengine lakini Omari kwa sababu ni mlemavu yeye ndio ambae hata akizungumza hatoaminika bhasi anabebeshwa ".
Omar anasema anakosa msaada licha ya kuendelea kujishughulisha na kilimo cha miche mbali mbali ikiwemo Mivinje, kutokana na kukosa soko, kutiliwa ng'ombe katika shamba na baadhi ya watu katika kijiji chao.
Comments
Post a Comment