CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WATOTO WALIOATHIRIKA NA UDHALILISHAJI WAANDISHI WA HABARI PAZENI SAUTI KUWASAIDIA.

NA AMINA  MOH’D, PEMBA. 

WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba wameaswa  kupaza sauti zao, katika kusaidia upatikanaji wa haki mbali mbali wanazoendelea kuzikosa watoto wanaofanyiwa udhalilishaji wa kijinsia  kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo, kukosekana kwa sheria maalumu inayosimamia masuala ya udhalilishaji pamoja na  ushahidi madhubuti na kupelekea kufutwa kwa kesi mbali mbali mahakamani kwa kuandika habari  na makala  mbali mbali.

Ameyasema hayo   Mratibu wa chama  cha Waandishi wa Habari TAMWA-Zanzibar kisiwani Pemba Fat-hiya Mussa Said alipokuwa akizungumza na  waandishi wa habari  huko katika ukumbi wa  ofisi hizo  Mkanjuni Chake  chake  katika mafunzo maalum kwa Waandishi juu ya kuandika changamoto zinazowakabili watoto walioathirika na vitendo vya udhalilishaji . 
         FAT-HIYA MUSSA SAID, MRATIBU TAMWA PEMBA
 "Bado  watoto waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia wanaendelea kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kukosa ushauri nasaha,kukosa fidia zao na kufutwa kwa kesi mbali mbali kutokana na kukosa ushahidi madhubuti  watetezi wa kuzisemea changamoto hizi  waandishi mnayo nafasi kubwa katika kuwasaidia kuzipatia ufumbuzi. "
         SITI HABIBU MUHAMMED, MKUFUNZI. 
Akitoa elimu juu ya sheria mbali mbali Siti Habibu Muhammed amesema serikali ya Zanzibar imeanzisha sheria mbali mbali mikataba ya kimataifa pamoja na  mikataba ya kikanda katika kulipatia ufumbuzi suala la udhalilishaji hivyo ni vyema  waandishi hao kuzitumia katika kuasemea mapungufu yanayopelekea kuongeza changamoto na  vitendo vya udhalilishaji kwa waathirika hao.

Nao baadhi ya waandishi wa habari   hao wamesema wataendelea kuzisemea changamoto hizo kwa kuandika habari na makaa mbali mbali  zitakazosaidia kuondoa changamoto hizo zinazoendelea kujitokeza kwa waathirika wa udhalilishaji.

Mafunzo hayo maalum yaluoandaliwa na Tamwa kwa Ufadhili wa Faundation for civil Society yamewashirikisha waandishi wa vyombo mbali mbali ikiwemo  Radio, Tv, Magazeti pamoja na mitandao ya  kijamii       


Mwisho 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.