BONANZA LA 5 LA UTALII PEMBA KURUDI TENA, WANANCHI WAASWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO MBALI MBALI.
Na Amina Ahmed Moh’d, Pemba.
BONANZA la 5 la Utalii Pemba (Pemba Tourisport Bonanza) kuanza Rasmi Tarehe 28 Mwezi huu wa 11 na kufikia Tamati Tarehe 3 Disemba ambapo wananchi kutoka maeneo mbali mbali Tanzania wameaswa kujitokeza kuchukua fomu za ushiriki wa michezo mbali mbali bila malipo yeyote.
Akitoa Taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari mbali mbali Mratibu wa kamisheni ya Utalii Pemba Hamad Amini Ali amesema lengo la bonanza hilo ni kuunga mkono juhudi zinazoendelea kufanywa na rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi katika kufanya utalii wa Kisiwa hicho kuwa endelevu pamoja kutangaza vivutio na michezo mbali mbali ya asili Iliyopo ndani ya kisiwa hicho na kuongeza idadi ya wageni wanaoingia kisiwani humo kwajili ya shughuli za utalii.
HAMAD AMINI ALI- MRATIBU KAMISHENI YA UTALII PEMBA.
Amesema tayari maandalizi kupelekea bonanza hilo maalum la kuhamasisha utalii wa kisiwa cha Pemba ambalo litafanyika katika wilaya zote kisiwani humo yameshakamilika ambapo jumla ya michezo 15 ya Asili inatarajiwa kuhamasishwa katika bomamza hilo pamoja na kufanyika kwa shughuli mbali mbali za kijamii.
Hata hivyo Mratibu huyo amewataka waandishi na wananchi maeneo mbali mbali kisiwani Pemba kujitokeza kwa wingi katika maeneo mbali mbali yatakayotumika kwajili ya michezo iliyoandaliwa katika bonanza hilo.
Kwa Upende wake Afisa Utalii Kutoka kamisheni ya Utalii Pemba Said Salum Ali amewataka wananchi kisiwani humo kuonfoa dhana ya utalii ni uhuni badala yake waendelee kuinga mkono serikali kupitia sekta hiyo kufanya utalii katika maeneo mbali mbali kwajili ya kuongeza kipato kitakachotumika kuongeza maenedeleo nchini.
SAID SALUM ALI-AFISA UTALII KASKAZINI, PEMBA.
Aidha Amesema kuwa Bonanza hilo limeandaa zawadi nono kwa washindi pamoja na washiriki wote ambao wanatarajiwa kushiriki katika michezo mbali mbali sambamba na kuendelea kusimamia maadili ikiwemo utalii unaoendana na uhifadhi wa mazingira ya kisiwa hicho.
Michezo hiyo inayotarajiwa kushindaniwa katika bonanza hilo maalum la Kuhamasisha utalii ni pamoja na Gwaride la Punda, ambalo litaanzia Tibirinzi Chanjaani na kumalizia Pujini, Pamoja na Mchezo wa ng'ombe, Mbio za baiskeli, kukimbia , mashindano ya kuogelea, Mpira wa fukwe,Taarabu asiliya, Mashindano ya dufu, mchezo wa bao, Ngoma, Mashindano ya ngalawa, Mchezo wa Ngware, Mashindano ya kula vyakula vya Asili, matembezi ya utalii wa kiislam, Usafishaji wa fukwe, sambamba na shughuli za wajasiriamali kwa akina mama kwa utaratibu na siku maalumu .
Maeneo yatakayotumika kwajili ya mashindano ya michezo mbali mbali ni pamoja na Puniji, Vuma wimbi, Micheweni, Msitu wa ngezi, Tibrinzi, Mkoani, pamoja na Tumbe.
Comments
Post a Comment