WAZEE WAGONJWA WAPATA FARAJA HII KUTOKA KWA MWAKILISHI NA MBUNGE WA JIMBO LA OLE.

Na, Amina Ahmed Moh’d - Pemba - 0719859184. 




JUMLA ya  Wagonjwa 15 Wamepatiwa Fedha kwajili ya Kusaidia Kupunguza Gharama za Matibabu ikiwemo kununua  Dawa ikiwa ni Msaada Maalum uliofanywa na Mwakilishi wa Jimbo La Ole Massoud Ali Muhammed Pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Juma Hamad Omar.
Wagonjwa hao ambao wanaendelea kupatiwa  huduma za matibabu Majumbani kutokana na  Uzee    wamepatiwa Msaada huo kufiatia ziara maalum ya kuwatembelea na kuwajulia hali    iliyofanywa na viongozi hao wakiambatana na kamati ya Siasa ya Jimbo hilo  Mapema Leo Asubuhi. 
Akikabidhi Fedha  hizo  Mbunge Wa Jimbo hilo Amesema Uongozi wa  Jimbo kwa Pamoja   umeamua  kufanya  ziara hiyo  na kutoa Masada  ili kusaidia  kuimarisha Afya zao na kurudi katika utekelezaji wa Majukumu yao  kama ilivyokuwa Awali.

 Aidha  Akizungumza  kwa niaba ya Mwakilishi wa jimbo la Ole Massoud Ali  Diwani wa Wadi ya Vitongoji Hamad Abdalla Hamad Amesema kuwa Uongozi wa Jimbo utaendelea kufanya hivyo katika kutunza Na kuthamini Mchango Uliotolewa na wazee hao walipokuwa na  Afya Imara Ikiwa ni pamoja na Mawazo mazuri ya  kuchochea  na kuhamasisha Maendeleo ndani ya Jimbo hilo. 

Hata hivyo  Uongozi huo umesema utaendelea kusaidia Zaidi  Huduma za Matibabu kwa wagonjwa hao Pindi zitakapohitajika  ambapo umewataka wauguzi wa wazee hao kuendelea Kutoa  mashirikiano  juu ya Hali ya  upatikanaji wa  huduma za matibabu yao ili kuendelea kuchangia Zaidi. 

 Wakizungumza Baadhi ya Wazee hao Akiwemo  Mbwana Ali Omar mkaazi wa Vikunguni, Haji Abdalla Ali Pamoja na Mchanga Hamad Bakari  Mkaazi Vitongoji wameushukuru uongozi huo  kwa kuwasaidia fedha hizo ambapo wamewataka Viongozi wengine kuiga Mfano huo wa kuwatembelea na kuwafariji wazee Wanaoendelea kujiuguza Majumbani maeneo mbali mbali. 
 
Jumla Ya Shilingi Laki 7 na 50 Zimetolewa  kwa Wagonjwa hao ambapo pamoja na kuwatembelea lakini pia uongozi huo Uliwaombea Dua  kuwafariji  Pamoja na kupoke Ushauri  juu ya  mambo mbali mbali waliopewa na Wazee hao ambapo kila mmoja Alikabidhiwa Jumla ya shilingi elfu 50. 

Mwisho. 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.