VIONGOZI WA JIMBO LA OLE WAPEWA KONGOLE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI MWAO.
NA, AMINA AHMED MOH’D- PEMBA. 0776859184
KAMATI ya Siasa Jimbo la Ole Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba Imesema Imeridhishwa na kasi ya Maendeleo iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Viongozi wa Jimbo Hilo katika Kuleta Maendeleo ya Huduma bora Kwa Wananchi ndani ya Jimbo hilo.
Akizungumza na Habari hizi Mara baada ya kumalizika Ziara Maalum ya kutembelea na kukagua Miradi mbali mbali iliyotekelezwa na Mwakilishi Massoud Ali Muhammed pamoja Mbunge wa jimbo hilo Juma Hamad Omar Mwenyekiti wa kamati hiyo ambae pia ni Kiongozi wa Madiwani Wilaya ya Chake Chake Hamad Abdalla Hamad amesema utekelezaji wa miradi hiyo imeleta Tija na Maendeleo kwa Wananchi katika kurahisisha huduma mbali mbali .
HAMAD ABDALLA HAMAD - M/KITI MADIWANI CHAKE CHAKE.
Kwa Upande Wake Mbunge Wa Jimbo la Ole Juma Hamad Omar amesema lengo la kuzipatia ufumbuzi changamoto sugu zilizokuwa zinawakabili wananchi katika Jimbo hilo ni kuboresha na kutatua Changamoto za Wananchi kama Ambavyo ilani ya Chama cha Mapinduzi Imeelekeza.
Aidha Akizungumza kwa Niaba ya Mwakilishi wa Jimbo hilo Massoud Ali Muhammed Diwani wa Wadi ya Vitongoji Chake Chake Hamad Abdalla Hamad amesema lengo la kutekeleza Miradi mbali mbali ni kusaidia kuwaondoshea usumbufu Wananchi wa jimbo hilo na kupata huduma bora.
Aidha kwa upande wake katibu wa Jimbo La Ole Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Yakoub Halfan Shaha Amesema kuwa Ziara hiyo ya kukagua miradi mbali mbali iliyofanywa na Mwakilishi pamoja na Mbunge wa jimbo ni kuangalia namna ya utekelezaji wa Ahadi zilizotolewa na Viongozi hao katika Kipindi cha Miaka 5 juu ya Utekekelezaji wa Ilani ya Chama.
Kamati hiyo Imetembelea na kujionea Miradi ambayo Tayari Wananchi ndani ya jimbo hilo wameanza kunufaika nayo ikiwa ni pamoja na Barabara za ndani , Ukarabati na ujenzi Skuli Za sekondari, Ujenzi wa Holi la Mitihani Sekondari, Upaatikanaji wa Maji katika maeno mbali mbali yaliopelekwa mabomba na Viongoz hao Huduma ya Umeme na kumalizia katika Soko la mboga mboga pamoja na Matunda la Ubaya Sikitu Lililopo Ole Kianga ambalo tayari Wafanya Biashara wameanza kutumia kwa Harakati Zao.
Mwisho.
Comments
Post a Comment