MKURUGENZI BARAZA LA MJI CHAKE CHAKE ATOA WITO HUU KWA WATOA HUDUMA MAKUNDI MAALUM, ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA KATIKA MAFUNZO YALIONDALIWA NA ZAYADESA.

NA- MARYAM MKAMBAYA, PEMBA. 

MKURUGENZI wa Baraza la Mji Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Maulid Mwalimu amewataka Watoa huduma wa Makundi maalum  wawe tayari kuyafanyia kazi kwa ari mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya Makundi hayo ili waweze kuepukana na maambukizi ya virusi vya ukimwi na walio navyo wasiweze kusambaza.

Ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wauguzi yaliyotolewa na Mradi wa ZAYEDESA katika ukumbi wa Samail Gombani .

Amewataka wauguzi hao wahakikishe wanakwenda kubadilisha jamii waweze kuondokana na kuwanyanyapaa  watu wenye uhitaji maalum ili waweze kujiona  ni sawa na watu wengine.

Nae Dokta Mahmud  Ibrahim Mussa mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa ajili ya Makundi maalumu kwa sababu ndio watu waliopo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Amesema kuwa maambukizi ya virusi vya ukimwi yapo chini ya asilimia moja kwa Wanzanzibari wote  lakini kwa Makundi maalumu yapo chini ya asilimia tano ambayo ni hatarishi.

Nae Raya Hakim Mohamed  Muunguzi kutoka hospitali ya chake chake amesema ipo Haja yakutolewa elimu kwa Makundi maalumu juu ya kujua fursa zao pamoja na haki zao na kujiona kuwa ni sawa na watu wengine.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.