WIZARA YA UTALII PEMBA YAONGEZA KASI KATIKA USHAJIHISHAJI WA UTALII KWA WOTE YAAHIDI KUONGEZA MASHIRIKIANO KWA WATU WA RIKA ZOTE

Na Amina Ahmed Moh’d   Pemba 

VIJANA Kisiwani Pemba Wameaswa kuzichangamkia Fursa zinazopatikana kupitia Sekta ya Utali iwa   aina mbali mbali  ili kiweza kujipatia kipato wao binafsi na kuleta Maendeleo kwa Taifa sambamba na kutembelea Pamoja  kutunza maeneo ya kihistoria yaliyopo.

  Ametoa Ushauri huo Mkuu wa Wilaya Wete  Hamad Omar Bakari    Alipokuwa Akizungumza nao Katika  Warsha  Maalum ya Uhamasishaji wa Utalii kwa Wote iliandaliwa na Wizara ya Utalii na mambo ya kale  Huko Katika Makumbusho ya kihistoria Chwaka Tumbe Mkoa Wa Kaskazini Pemba. 
 HAMAD OMAR BAKARI - MKUU WA WILAYA YA WETE 

 Amesema  Utalii umekuwa Na Fursa nyingi zitakazosaidia  kuwapatia kipato binafsi na Taifa  Endapo wataamua kuzitumia  kwa kufanya shughuli mbali mbali   ikiwemo kuutangaza Utalii  Wa kihistoria uliopo kisiwani Pemba.

 Akizungumza  katika  Warsha  hiyo Ofisa Mdhamini  wizara ya Utalii na mambo ya kale Pemba Zuhura Mgeni Othman   amesema Wizara hiyo
 itaendelea kushirikiana  na vijana, Wajasiriamali pamoja na wananchi mbali mbali  katika  kuimarisha na kutangaza utalii  Wa aina mbali mbali. 
  ZUHURA MGENI OTHMAN - AFISA MDHAMINI WIZARA YA UTALII NA MAMBO YA KALE PEMBA. 
 wakizungumza baadhi ya vijana  wajasiriamali na wanafunzi ambao wamehudhuria katika warsha hiyo ya kuhamasisha utalii kwa  wote  wameipongeza wizara ya utalii Pemba kwa kuendelea kuhamasisha jamii juu ya utalii wa ndani  ambapo wamesema kupitia hamasa hiyo wameweza kujifunza mambo mbali mbali ya kihistoria. 


 Warsha hiyo imehudhuriwa na  wadau mbali mbali wa Utalii  wakiwemo wadau wa hoteli, waongoza wageni, watu maarufu katika kijiji cha chwaka, Wajasiriamali,   wanafunzi pamoja na mtalii wa  kigeni  kutoka Nchi ya Holanzi ambapo  Warsha hiyo iliambatana na kutembelea makumbusho hayo yenye  historia   mbali mbali  ya chwaka Tumbe.


 Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.