WAZANZIBARI WAASWA KUUNGANA NA TAMWA-ZANZIBAR KUHUSU UONGOZI KWA WANAWAKE.
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA.
BAADHI ya Viongozi wa Dini ambao ni Miongoni mwa Wanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Kisiwani Pemba wamewataka wazanzibari Kuungana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar TAMWA katika kuhakikisha Usawa wa kijinsia katika Ngazi za maamuzi Unafikiwa ifikapo 2025.
Akizungumza na Habari hizi Mwanaharakati wa Maendeleo ya Wanawake Pemba Pascal Nkuba Ambae pia ni Mchungaji wa kanisa Redeemed Gospel Church (RGC) lililopo Minazini Chake Chake Amesema kutokana na Nia na Dhamira Njema inayoendelea kuoneshwa na Taasisi hiyo Wazanzibari wote wanaowajibu kuunga Mkono Juhudi hizo ambazo lengo lake ni kuongeza kasi ya Maendeleo kwa Wanawake.
MCHUNGAJI, PASCAL NKUBA - RGC MINAZINI CHAKE CHAKE.
"Tamwa imekuwa Ikitoa Elimu kwa watu wote maeneo mbali mbali na Makundi yote kuhusu Uongozi kwa wanawake kwa Ishara hiyo tunao Wajibu wa kuiunga Mkono kufikia Malengo hao abayo ni mema kwa wanawake.
Aidha alisema kuwa ipo haja kwa wadau na Makundi yote ambayo yamefikiwa na Taasisi hiyo kuendelea kuhamasisha Jamii juu ya ushiriki wa wanawake katika Uongozi na kuendelea kudai haki hiyo katika nyanja mbali mbali.
"Binafsi nikiwa kama kiongozi wa Dini wa RGC naendelea kutoa elimu kwa waumini wangu pamoja na kukemea vikali kumkandamiza Mwanamke kwa dhamira ya kubaki nyuma kimaendeleo, labda kwa kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, Au kunyimwa fursa ya kushiriki kutoa maamuzi na kumekuwa na mabadiliko kidogo kidogo wadau wa makundi ambayo yamefikiwa na Tamwa Iendeelee kutoa elimu ambayo wamepatiwa "
Kwa Upande wake Fatma Hamad ambae Mwanaharakati na Mwandishi wa habarikisiwani alisema kuwa licha ya jamii kupata Uelewa ipo haja kwa Taasisi hiyo kuweka mpango mkakati ambao utasaidia kuikumbusha jamii juu ya suala la uongozi kwa wanawake kila siku.
"Tamwa na Taasisi nyengine Waendelee kutumia vyombo vya Habari vya aina mbali mbali, ikiwa ni radio, magazeti, mitandao, vipeperushi kufikisha ujumbe ambao Makundi yote yatakuwa na kauli moja kuelekea 2025 hii itasaidia kuongeza hamasa kwa jamii Alisema.
" Mfano kuweke Kauli mbiu ambayo itakuwa ni endelevu Lakini itafikiwa na makundi yote na itasikika kwa wote mabadiliko yatafikiwa tu".
Akizungumzia Suala hili Sheikh Suleiman Said kutoka Mkanjuni ChakeChake Amewaasa waumini wanawake Kuitumia fursa hizi za uongozi kwa kufuata mafundisho ya Dini bila kuenda kinyume.
" Awali Waliowengi walikuwa wanaielewa vibaya hii Dhana ya Uongozi wapo ambao walikuwa wanashindwa kutofautisha ni upi uongozi unaopigiwa kelele na Asasi hii ya Tamwa na Asasi nyengine lakini niseme tu Kila mtu anaowajibu wa kuwa kiongozi akina uongozi ulioharamishwa kwenu sio huu ambao Tamwa wanaupigia kelele uwena usawa tumieni fursa".
Kwa Upande wake Fat hiya Mussa Said Ambae ni Mratibu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Ofisi ya Pemba amesema Muamko kwa Jamii umeongezeka kufuatia elimu inayoendelea kutolewa juu ya masuala hayo ya uongozi na haki sawa kwa wanawake na wanaume ukilinganisha na Awali.
"Hali imebadilika awalo tulipoanza kutoa elimu juu ya sala hili wadau wakiwemo viongozi wadini walikuwa wakali sana hawakuwa wanataka kutoa hata mashirikiano yakutosha waliona kama tunapotosha Jamii lakini baaa ya kujengewa uelewa Tunashukuru wamekuwa wakituunga mkono na kusaidia kuondoa zile fikra Potofu a mawazo Mgando ambayo yamekuwa yamo katika akili za watu "
Aidha Mratibu huyo amewataka wananchi kisiwani Pemba Kuendelea kuunga mkono juhudi hizo zinazofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar kwa kushirikiana ma Wadau na Taasisi mbali mbali yenye lengo la kuleta Mageuzi ya fikra na kukuza Uchumi wa Wanake.
Mwisho.
Comments
Post a Comment