WANAWAKE KISIWANI PEMBA WATOA YA MOYONI UCHAGUZI WA MAJIMBONI NAFASI MBALI MBALI.



NA - AMINA AHMED MOH’D  PEMBA. 

WANAWAKE watiania kuogombea nafasi za uongozi wamesema moja ya changamoto kubwa inayowarudisha nyuma kuwania nasafi za uongozi katika changuzi mbali mbali zinazofanyika ni uwepo wa vitisho wanavyokumbana navyo kutoka kwa wagombea wenzao wanaume .

Wamesema vitisho hivyo huwafika wao, pamoja na familia zao na wakati mwengine wagombea hao huwafuata wazazi wao au waume zao ili kukatazwa kuachia nafasi hiyo aliyogombea.


Wakaizungumza na habari hizi kwa nyakati Tofauti  baadhi ya Wanawake wanaotarajiwa kugombea nafasi za uongozi na siasa katika mchakato wa Kidemokrasia Kisiwani Pemba, Wamesema Changamoto  hiyo licha ya kuendelea kupata mafunzo mbali mbali namna ya kuikabili lakini bado imekuwa ikiwarudisha nyuma kutimiza ndoto hizo walizojiwekea. 

Mmoja ya watia nia hao Asha Ali Abdalla kutoka chama cha ACT-Wazalendo, alisema suala la vitisho ndani ya vyama vimekua vikiwavunja moyo wanawake wengi na wengine hulazimika kuachia ngazi ili kunusuru maisha yake au familia yake.

“Nilipo tangaza nia ya kuingia jimboni, baadhi ya watu waliweza kunifata na kumtaka kuwamchia mtu kwa mwaka ule, lakini sikurudi nyuma nikachukua fomu, mwisho wa siku walifika mpaka kwa mama yangu na kumwambia anikataze,”alisema.

 Asha Said Salum kutoka Chadema, alieleza kuwa baadhi ya  viongozi wa juu wa vyama  wamekuwa na tabia ya kuwakumbatia  watia nia wenye uwezo wenye uwezo ambao kwa asilimia kubwa wamekua ni wanaume na  kuwacha wanawake wenye nia thabiti ya kuwasaidia wanawake na watoto na maendeleo kwa Taifa jambo ambalo  lisipodhibitiwa litaendeleza kukuza mfumo dume katika nyanja za Siasa. 

“Wanawake wengi wanania thabiti ya kugombania nafasi za uongozi,  mimi ni mmoja wao lakini viongozi wa juu wa vyama h ndio wanaorudisha nyuma na kufuta ndoto tulizo nazo , huu ni mfumo dume amboa umezoeleka kwenye baadhi ya vyama tunatamani wadau  na Serikali waweke sheria maalum itakayoweka usawa  katika vyama juu ya suala hili,”alisema.

Kwa upande wake Maryam Abdalla Salim kutoka ACT-Wazalendo, aAlisema uzalendo kwa wanawake  Wenyewe ndio silaha kunwa ya uthubutu na  utayari, wakati wanapoamua kuingia kugombea nafasi za  Majimboni.

Stara Khamis Salum kutoka CCM Wilaya ya Chake Chake, alisema bado wanawake wanakumbana na masuala ya ubaguzi wakati wa chaguzi zinapofika, hivyo wanapaswa kushirikiana na kufikia ndoto zao bila kuqeka Makundi ndani ya vyama yatokanayo na wanawake kwa wanawake wenyewe .

Hata hivyo aliwataka wanawake wenzake wenye nia ya kuingia Majimboni, kuhakikisha wanatengeneza ngome  zao mapema ili wakati utakapofika inakua ni rahisi kwao.

 Akizungumzia suala hili  la Uongozi kwa wanawake Mmoja kati ya  Mwanaharakati wa masuala ya wanawake Kisiwanai Pemba Sabahi Mussa Said, alisema  Mchango mkubwa Walionao wanawake katika Masuala ya kuleta Maendeleo ya  Jamii  na Nchi ni kuhakikisha wanawake wanachangia  katika maendeleo  kwa kushiriki na kugombea na  kudai nafasi za Uongozi  bila woga. 

Sabahi Alisema wanawake wanaumizwa na suala zima la maendeleo tafauti na wanaume, kwani wao ndio wanaohangaika kwa kutafuta huduma mbali mbali ikiwemo kijamii.

Hafidh  Abdi Said, ni Mkurugenzi wa   Jumuia ya utetezi wa kijinsia na Mazingira Pemba( Pegao) ambayo imekuwa mchango mkubwa katika kubadilisha Wanawake kisiwani Pemba kuendana na Mabadiliko na kuwawezesha uthubutu wa kushiriki mambo mbali mbali Ametoa wito kwa wanawake wambapo Alisema kuwa

"Wakati wakubadilika sasa na suala la uongozi sio la mtu mmoja lazima kuwe na Mashirikiano ya pamoja Pegao tunaendelea kushirikiana na taasisi mbali mbali  Ikiwemo Tamwa kuwajengea uwezo wanawake.


Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.