MAANDALIZI YA MAPEMA CHACHU YA VIONGOZI BORA WANAWAKE NA WADAU NA SERIKALI KULIANGALIA SUALA HILI KATIKA KULITILIA MKAZO KUANZIA SKULI ZA AWALI MSINGI SEKONDARI HADI VYUO VIKUU.

NA AMINA AHMED MOH'D. PEMBA 

         KUNA USEMI USEMAO ‘mtoto mfunze angali mdogo’ na wengine husema ‘Kambare mkunje bado angali mbichi’ misemo hii ya kiswahili ina maana sawa na kikawaida waliosema wahenga huwa ni maandishi yalisadifu maana.

Licha ya wadau  Taasisi na Serikali  kuendelea kupambana katika kuibua  na kwaandaa  wanawake ambao watakuwa viongozi bora lakini Ipo Mifano ya kuigwa na vijana pamoja na wanawake wenye malengo  katika kufikia uongozi . 

Wapo waliodiriki kusema sio Dhambi kuiga Maendeleo kuoitia Waliofanikiwa. 

Serikali za wanafunzi ni Moja ya chuo cha kujifunzia Uongozi wanafunzi wanapokuwa Skuli kwani huongoza wanafunzi wenzao mithili ya wale Wazee wanavyongoza wananchi wenzao.

Katika Skuli iwe ya Chuo, Sekondari , Msingi n,k, huwa na Uongozi wake kwa nafasi mbali mbali mfano wa Serikali ambapo kama mwanafunzi atapitia nafasi hizo kwa muda mrefu huwa maejifunza au amaepata darasa tosha la Uongozi .

Na hivyo ndio alivyojifunza  Msichana jasiri  Rushda Khamis Kassim (28)   ambae kwa sasa hivi ni Makamo mwenyekiti wa  mabaraza ya vijana Taifa  kwa upande wa Zanzibar na kuliongoza vyema baraza hilo kwa vile alipitia katika maadalizi ya uongozi akiwa Skuli.

Rushda , alianza  harakati za uongozi na kumjenga tokea  akiwa Skuli ya Msingi akaendelea nao akiwa sekondari elimu ya juu na hadi leo licha ya kuwa ni mwalimu lakini pia ujasiri katika uongozi umemsaidia kufika mbali kimendeleo.

Katika harakati zake za kuongoza makundi ya watu alipata fursa mbali mbali za kutembea   kupitia ujasiri wake na uthubutu na msimamo kama mwanamke kijana ambapo harakati za uongozi zimebadilisha maisha yake kwa ujumla.

Serikali ya wanafunzi ni mfumo ulioanzishwa katika Skuli  na Vyuo mbali mbali vya binafsi na Serikali ambao lengo lake ilikuwa ni kusaidia na wanafunzi kuwa na sehemu ya kupeleka malalamiko yao ,kujenga nidhamu na heshima kwa wanafunzi na walimu wao .

Mfumo wa Serikali ya wanafunzi maskulini haina tofauti na mfumo wa Serikali za kijamii kuanzia utendaji wake , miiko na wajibu katika uongozi .


Kama ambavyo Rais au waziri  katika nchi anawajibu wa usimamia  ,kukemea raia katika Serikali ili mambo yaende sawa basi ni hivyo hivyo mfumo wa uongozi katika Skuli na Vyuo  ulivyo utendaji wake.

Rushda Khamis Kassim (28) alianza harakati za uongozi akiwa katika Skuli ya msingi Madungu iliyopo Mkoa wa kusini Pemba akiwa kiranja wa darasa.

Anasema  baada ya kufika sekondari akiwa katika Skuli ya Sekondari Shamiani Chake chake aliweza kushika nyazifa mbali mbali za uongozi kupitia Serikali ya wanafunzi .

“ Wakati nikiwa kiongozi wa Skuli nilikuwa najiamini wala sikuona kama ni mwanamke nikajilegeza nilitekeleza majukumu yangu kama kiongozi wa kweli kweli, kumbe pale nilikuwa najifunza na sasa ninauwezo wa kuongoza pahala popote”, alisema.

Anasema wakati anaanza kuongoza wanafunzi wenzake pale Skuli kuna watu akiwemo Mwalimu wake wa darasa  aligunduwa kuna kitu ndani yake ni mwalimu wake wa darasa wakati huo yupo madarasa  ya msingi na mara baada ya kugundua kipaji hicho alianza kumshirikisha katika mambo mbali mbali.


 Anaeleza kuwa wakati yuko skuli aliweza kuingizwa kwenye  michezo ya kuingiza,midahalo, ngonjera na humo mote alisimama kama kiongozi kwa kuwakilisha makundi hayo katika matamasha ya elimu bila malipo.

"Kiukweli harakati hii ya Uongozi sikuianza tu kuwa kiongozi wa juu hapa Zanzibar kama ambavyo nipo sasa wala sikuianza kwenye kuongoza kundi kubwa la watu bali nilianza kuongoza makundi madogo madogo nikiwa skuli kwa  awamu tofauti tofauti", alisema .

Anafahamisha wakati akiwa Skuli kidato cha pili (Form two) alikuwa kiongozi katika Serikali ya wanafunzi kama  kiongozi na msimamizi wa maadili, nafasi ambayo alidumu nayo huku akiwa kiongozi wa darasa lake lenye wanafunzi 81 kwa wakati huo.

Anasema haikuishia hapo baada ya mwaka kumaliza na kuingia mwaka mwengine na madarasa mengine pia aliweza kugombea nafasi ya makamu wa Rais hapo Skuli akiwa (form three) ambapo alikosa   lakini bahati iliyonjema alipata uongozi   wa Serikali ya wanafunzi kwa kuchaguliwa na Rais wa skuli kuwa waziri wa mazingira katika Serikali hiyo . 

“Nikiwa form four sasa nilipata tena bahati ya kuwa Waziri wa fedha usisahau mwandishi nyazifa hizo nilikuwa nazitendea haki hakujawahi kutokea malalamiko yeyote juu ya utendaji wa kazi wangu na darasani nilikuwa sishuki kimasomo na namba yangu ya matokeo ilikuwa ni hapo hapo kati ya moja mpaka kumi sijawahi kuzidi mpaka nimeondoka Skuli kuenda kuendeleza masomo yangu Chuoni”, alieleza.

 Anaeleza kuwa alipomaliza Skuli aliingia katika chuo cha  ZCBE na huko nako wanafunzi wenzake  na Waalim walimpendekeza kuwa kiongozi naalikubali na akaanza kushajihisha wenzake kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ambazo zilitolewa hapo  Chuoni.

Anasema  lakini chakushangaza waliowengi pale wakiwemo watu wazima zaidi yake walimwambia wanataka awe yeye  Rushda ndio kiongozi usishajihishe wengine yeye  wanahisi anaweza kuisimamia nafasi hiyo kwa hiyo achukuwe nafasi ya ukatibu mkuu ambayo ilikuwa ni kubwa na muhimu  hapo chuoni.

“ Kweli nilichukuwa kwa vile ni kundi kubwa sana ambalo lilinikubali na kunipendekeza  nafasi hiyo sikuigombea bali nilipendekezwa kwa kura za ndio na hapana alisema sio kwa hivyo kura na ndio zilikuwa nyingi kwa asilimia 100 kwa wanafunzi wote", alisema.

Anaeleza kuwa baada ya kuwa katika Serikali ya wanafunzi hapo chuoni alishukuru alishirikiana vyema na viongozi wengine na waliongoza vizuri na alipata kujifunza mambo mengi mengi zaidi hapo chuoni kwa sababu kule Skuli alipoanzia ni kama ilikuwa mzaha tu mfumo wa uongozi kwake.

Anasema kuwa  alishika nyazifa hiyo kwa muda wa miaka mitatu la hapo  chuoni mpaka amemaliza diploma akakabidhiwa  Cheti  maalum cha heshima ya uongozi kwa vile ni yeye pekee ambae alihudumu kwa muda mrefu . 

Anafahamisha kuwa baada ya kumaliza chuo harakati hizo za uhamasishaji zilihamia katika jamii alikuwa mwanaharakati alihamasisha jamii alishiriki kazi mbali mbali za kijamii ikiwemo usafi, kushiriki katika sherehe mbali mbali, kwahiyo aliporudi katika jamii hakuwa mpweke alijikuta yupo na kazi nyingi za kufanya katika jamii yake.

                     

Baada ya hapo sasa cheti changu kilikuja na kwa Bahati iliyonjema sana kilikuja na matokeo mazuri nilipata first class ya 4 point 5 GPA Fani y Human Resource Menegment nilijikuta nmepasi vizuri na nilipoapata cheti changu na nilijitolea ktika taasisi zisizo za kiserikali kufanya kazi ya kile nikichokisomea na niliamua kujitolea katika taasisi binafsi kutokanaa na kile nikichokisomea sidhani kma katik tasisi za serikali kuna uwezekano wa kufanya kazi za kujitolea kwa fani hii ya usimamizi wa rasilimali watu . 


 Licha ya kuwa na fani Maalum niliosomea lakini pia ninafani ndogo ndogo ambazo nimesomea kwa muda mfupi kama vile fani ya ueleimishaji jamii Pear educater .


Wakati huo nasubiri vyeti vyangu vya kumalizia chuo sikubweteka mpka vije ndio nitafute ajira bali niliendelea kuzitumia zile tasisi ambazo zilikuwa zinanitumilia nikiwa mwanafunzi katika ueleimishaji jamii na nikiendelea kuielimisha jamii yangu. 


 Nilienda Kujitolea SOS na hapo nilipata uzoefu na fursa mbali mbali bhasi huko nilifanya kazi na nilifanya kwa vile uongozi ulinipokea na kunikabidhi jukumu la kuzisimamia familia 75 na katika familia hizo nilipewa jukumu la kuhakikisha watoto wanarudi shuleni ambao wlishakatisha masomo kutokna na sababu mbali mbali nilifanya hivyo na kwa kushirikiana na wenzangu tulilifnikisha hilo . 

RUSHDA NI NANI KISWANI PEMBA 

Rushda ni mwanamke wa kwanza kuwai kushika na kutumikia nafasi hiyo ya Mkamo mwenyekiti baraza la vijana Taifa Zanzibar. 


" Awali uongozi wote wa ngazi za juu kwa hapa kisiwani pemba haujawahi kushikwa na mtu yyote yule najivunia kama mwanamke kushika nafasi hii kwa mara ya kwanza hapa kwetu kisiwani alisema". 

NI IPI SIRI KUFIKA HAPO ALIPO SASA MAKAMO MWENYEKITI BARAZA LA VIJANA. 

"Awali sikujijua nitaenda kuwa nani baadae katika baraza la vijana kwa vile nilikuwa mtu wa kawaida tu ila nilikuwa ni mtu ambae ujasiri na uthubutu wangu nilijaribu kuomba nafasi mbali mbali kabla hii niliopo sasa" 


  Aliendela kusema "Kwanza Nikujiamini pili ni kuishi kwa ndoto zangu kwa sababu hii nafasi niliipigania Nilionesha uthubutu na ndipo nilionekana kwamba kumbe kweli naweza kuitendea haki nafasi na ndipo mnamo mwezi wa 5 2021 rasmi nilichaguliwa kuhudumu nafasi hii ila haikuwa rahisi kwa sababu waliowengi walikuwa wanatamani kufika hapo nilipo mimi kwa sasa". 


 

"Kiukweli nimeanzia nikiwa memba wa kawaida wa baraza la vijana zanzibar kwa upande wa pemba lakini wilaya ya chake chake, nilikuwakama mjumbe wa kawaida katika baraza hilo. 

Baraza la vijana Taifa limezishwa kwa mujibu wa sheria iliyotungw na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Ambapo sheria hii ilijulikana kama Sheria ya Kuanzisha Baraza la Vijana la Zanzibar.

Ambapo utendaji wake baraza hilo utaanza kuanzia ngazi

ya Kitaifa hadi ngazi ya Shehia lililoanzishwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria hiyo Ambapo mwanachama wa baraz atakuwa na moja kati ya haki hizi kisheria

 haki na wajibu ufuatao 

 Kuchagua na kuchaguliwa;

 Kutoa maoni, mapendekezo na ushauri kwa Baraza na kufikishwa kwa serikali. 

" Mabaraza ya vijana yameanzishwa kuanzia ngazi ya shehia wilaya Mkoa hadi Taifa lengo ikiwa ni kufanya Shughuli mbali mbali za vijana ikiwa ni pamoja kuwajengea uwezo vi juu ya masuala h ya uongozi. 

Mwaka 2021 jumla ya wanawake watatu 3 tu wameshika nafasi za uongozi za juu katika baraza hilo ambalo linaundwa na kushikiliwa na watu saba kwa nafasi za juu za kitaifa huku mabadiliko ya kiutendaji yanafanyika kwa mfumo wa upigwaji wa kura ambapo kiongozi ndani ya baraza hilo anaweza kuhudumu kila baad ya miaka mitatu na kuwa na uhuru wa kugombea zaidi ya mara moja ni kila baada muda huo uliowekwa wa kufanya mabadiliko. 


Endapo Maandalizi ya Mapema yatafanyika uwezekano wa kupat idadi kubwa ya wanawake katika vyombo vya Maamuzi itaongezeka katik nyanja zote za Maendeleo kwa Rika zote  Alimalizia Rushda Khamis Kassim . 

Mwisho. 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.