MAABARA YA AFYA JAMII KISIWANI PEMBA YAFUNGLIWA RASMI USUMBUFU WA KUCHUNGUZA MAGONJWA NJE YA KISIWA HICHO SASA BHASI.

Na Amina Ahmed Moh’d Pemba. 

WIZARA ya Afya Zanzibar leo hii imepokea na  kuzindua Rasmi Maabara ya Afya jamii kisiwani Pemba  ambayo itasaidia kuchunguza magonjwa mbali mbali  kwa wakati  na uhakika jambo ambalo lilikosekana  awali kisiwani humo na kupelekea usumbufu   katika kuchunguza magonjwa mbali mbali.
Maabara hiyo ya kisasa ambayo imegharimu Shilingi Bilioni 3. 5 Fedha za Tanzania  hadi kukamilika kwakwe  ikiwa ni Utekelezaji wa Mradi  American Rescue plan   Act of 2021 ARPA  ambao unatekelezwa na shirika la Usimamizi na Maendeleo ya Afya Menegment and Development for Health (MDH) kwa kushirikiana na Unicef ,  Pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiwa ni Ufadhili wa  Shirika la  (U. S. CDC) 

  Akizungumza katika Ghafa hiyo Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui Amewataka  Watendaji wa wizara hiyo Pemba  kuitunza Maabara  hiyo na vifaa  vyake ili viweze kusaidia  na kufikia lengo lililokusudiwa la kufanyika shughuli za Uchunguzi na  upimaji kwa wakati  na ubora  unaoendana na kasi ya  Sayansi  na Teknologia.

 Aidha Mazrui amelishukuru na kulipongeza shirika la( MDH) kwa kuendelea kuwa  na Mchango Mkubwa  katika kuimarisha   Na kusaidia sekta ya Afya  hususan katika upatikanaji wa uhakika juuYa Huduma za afya  inazohitaji  Uchunguzi wa Magonjwa mbali mbali  na  li kuimarisha Uchumi wa Zanzibar na kuongeza  Kipato kupitia Sekta ya Utalii.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kisiwani Pemba Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud Amesema Maabara hiyo itasaidia kupatikana huduma za uchunguzi  kwa haraka kwa wananchi wa kisiwani humo na kuondolea usumbufu wa kufata huduma za uchunguzi  wa Magonjwa nje ya kisiwa hicho. 

Akizungumza kwa Niaba ya Shirika la Usimamizi na Maendeleo ya Afya ( MDH)  Daktari  David Sando amesema  shirika hilo limedhamiria kuondosha Changamoto za Upatikanaji wa Huduma za Uchunguzi  wa Magonjwa ya kijamii kisiwani Pemba . 

 Nae Kwa upande wake  Said Muhammed Ali Amabae ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Maabara ya Afya jamii kisiwani Pemba Ameahidi kutumiwa vyema Maabara na vifaa katika kuboresha afya katika Jamii kisiwani Pemba. 



Ghafla ya Makabidhiano na Ufunguzi wa Maabara hiyo  imefanyika Mapema leo huko  Wawi Chake Chake   ambapo maabara hiyo inatarajiwa kutumika kwa shughuli za Upimaji wa uchunguzi wa Magojwa mbali mbali ya wananchi Kusini na Kaskazini  Pemba .

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.