UVUVI WA CHAZA KATIKA SHEHIA YA KIKUNGWI NI MOJA KATI YA SHUGHULI INAYOWAKOMBOA WANAWAKE .

NA SALMA KHAMIS.UNGUJA


KATIKA kujikomboa na hali ngumu ya maisha na kuondokana na utegemezi,Wanawake wa Shehia ya kikungwi Wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja wameamua kujiimarisha kwa kuunda kikundi cha uvuvi wa chaza kinachoitwa "kwanini tushindwe" lengo ni kujikomboa na umaskini. 

Kikundi hicho ambacho kina idadi ya wanachama takriban ishirini(20) na kipo zaidi ya miaka (13) sasa. 

Wanawake hao wameamua kufanya harakati hio kupunguza ukali wa maisha na kuacha dhana potofu ya kua mwanamke ni tegemezi. 

Pia wamesema shughuli hio ya uvuvi wa chaza  inawanufaisha sana kupata mahitaji yao ya kila siku na kuwapatia watoto wao haki zao za msingi kama vile kupata elimu na mahitaji ya lazima. 

Vile vile wavuvi hao hufanya shughuli hiyo kwa kuvuka kwenda visiwani na kazi yao kuwa ngumu pale hali ya hewa inapofika kipindi cha mawimbi makubwa na upepo mkali na kupelekea baadhi ya siku kutokufanya kazi mpaka hali ya hewa itakapotulia .

Licha ya wanawake hao kufanya shughuli hiyo kwa muda mrefu sasa lakini wanahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu kutokana na changamoto inayowakabili ya  ukosefu wa soko la kuuzia bidhaa zao. 

Wanaporudi pwani hulazimika kukaa pembezoni mwa barabara sehemu ambayo sio salama kwa maisha yao na pia hupunguza thamani ya ubora wa bidhaaa yao hiyo. 

Hivyo wameiomba serikali kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu kwa kushirikiana na halmashauri kuwajengea soko ili kufanya kazi za kuuza bidhaa katika ubora unaohitajika pia wananchi wanaokaaa katika shehia ya kikungwi nao watafaidika na huduma hiyo na kupunguza ukosefu wa ajira pamoja na kuongeza pato la Serikali 

       "Kwa muda mrefu sasa tunafanya kazi hii kwenda kuvua chaza baharini na kuja kuuza mtaaani na tunashkuru kazi hiii inatusaidia sana katika kuendeleza maisha yetu kwani wengine sisi ni wajane tunashulikia familia, tumejenga pia nyumba zetu kupitia kazi hii hiii na bado tunaendelea nayo."
    Waliendelea kusema
      "Lakini sasa kinachoturudisha nyuma ni ukosefu wa sehemu maalumu ya kuuza bidhaa zetu na tunaporudi pwani tunakaa barabarani na hiyo ni hatari kwetu kwani baadhi ya madereva husimamisha magari chini ya miguu yetu na wengine hata kuturushia maji machafu, hivyo tulikuwa tunaiomba serikali watujengeee soko ili tuweze kuwa na sehemu salama ya kufanya biashara zetu."
    Wamesema Wavuvi.

 sheha wa shehia ya kikungwi Mohd Haji Ushahidi amesema anatambua kuwepo kwa kikundi hicho ndani ya shehia yake na kikundi hicho kinajitahdi na kinafanya kazi kubwa katika kukuza uchumi wao na wa nchi.
      
"Natambua uwepo wa kikundi cha ushirika wa chaza katika shehia yangu na najaribu kuwatafutia njia ya kupata misaada lakini bado mungu hajajaalia. "
   Ameendelea
"Na kuhusu malalamiko ya soko tayari tushayafikisha Halmashauri na tayari wako katika mipangilio ya kuwajengea soko kuweza kufanya biashara zao. "
    Ameendelea kusema
"Pia nawaomba wenye uwezo kuwasaidia wavuvi hao kwa nyenzo na taaluma ili kuwaboreshea chaza zao ziweze kua bora zaidi na kuuzwa nje ya nchi" .
Alisema sheha 

Kuna hatua zipi zinazochukuliwa na baraza la mji Wilaya ya kati katika kuwasaidia wanawake wanaovua chaza kuondokana na hali hiyo .Mkurugenz wa Baraza hilo Salum Mohd Abuubakar anafafanua.
  
      "Tulienda tukaonana nao na tukafanya mazungumzo mara nyingi na soko hilo tumeliingiza kwenye mpango wetu wa fedha ulionza mwezi Julai 2022 na tutajenga soko kubwa la wafanya biashara ya mazao ya baharini, taratibu za awali zote zimeshafanyika ikiwemo kuandaa michoro,kutafuta mkandarasi na tushatangaza zabuni ya ujenzi  wa soko hilo.
Ameendelea kusema
    Jumla ya fedha taslim shilling million mianne zimetengwa na Halmashauri Baraza la Mji Wilaya ya kati katika ujenzi wa soko la biashara ya mazao ya baharini huko kikungwi."
Amesema Mkurugenz 

Kwa vile serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Mheshimiwa Dk Hussein Ali mwinyi imedhamiria  kutumia uchumi wa buluu kuimarisha uchumi wa nchi na wanachi . Katika kutatua changamoto inayowakabili wavuvi hao wa chaza Wizara ya Uchumi wa Buluu kupitia mkurugenz wa Idara ya maendeleo ya uvuvi na mazao ya Baharini Dk Salum Soud Hamad anaeleza mipango yao .
         
          "Serikali ya awamu ya nane imewekeza msisitizo katika uchumi wa bluu kwaio wavuvi wa chaza nao ni wadau wetu muhimu katika uchumi wa buluu na tunaona sasa kuna haja ya kuboresha mazingira yao wanayofanyia biashara kwani ni hatarishi kwao wenyewe."
Ameendelea
   Tumezingatia sana mambo mkuu matatu, kuwapatia elimu ya kuboresha kile walichokua nacho,kuwatafutia masoko ya uhakika na kuwatafutia mitaji kwa sababu naamini chaza ni moja ya bidhaa muhimu sana kwa Zanzibar lakini bado haijawekewa nfumo mzuri wa biashara"
    Amesema Mkurugenz. 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye Dira yake ya maendeleo ya 2050 miongoni mwa yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na sera ya uchumi wa buluu .

Katika dira ya maendeleo ya mwaka 2020 ambayo ilitekelezwa ndani ya miaka 20 kutokea mwaka 2000 hadi mwaka 2020, Serikali imefanikiwa kufikia hadhi ya uchumi wa kati wa kiwango cha chini (Lower-Middle Income Status )ambapo imeshuhudiwa uchumi ukikua kwa kiwango cha 7%ambayo sio mbali sana na lengo la ukuaji wa kati ya 9%na 10%. Hivyo dira ya maendeleo ya mwaka 2050 imelenga kufikia hadhi ya uchumi wa kati wa juu (Upper-Middle income status)na uchumi wa buluu ukiwa ni kupaumbele kama silaha ya kuchochea mafanikio hayo. 

SALMA KHAMIS 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.