UKOSEFU WA USAFIRI WA MELI YA TANGA PEMBA WANANCHI WAMLILIA RAIS KUTOLIFUMBIA MACHO.

NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA 

WANANCHI Wilaya ya Wete  Mkoa wa Kaskazini Pemba Wamemuomba Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi Kuwasaidia  Usafiri wa uhakika  ambao utawarahisishia  huduma za usafiri  kutoka Pemba  kwenda Mkoani Tanga kwa shughuli  zao mbali mbali ikiwemo  Kufuatilia ununuaji wa bidhaa za Biashara

 Wametoa Ombi hilo  Huko katika Bandari ya Wete  Mkoa wa Kaskazini Pemba walipokuwa wakizungumza na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo iliyifika Bandarini hapo kwajili ya kutoa Elimu kwa wananchi  Waliokamatwa kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo  wakisafiri kuelekea Mkoa wa Tanga   kupitia Bandari zisizo Rasmi   kwa kutumia Majahazi  ya Mizigo. 

Walisema kutokana na kukosa usafiri  wa Uhakika wa kutumia Hulazimika kupanda Majahazi   ya Mizigo  Na kulazimika kushuka Bandari  zisizo Rasmi   ambapo hupelekea kuhatarisha Maisha yao  na kupelekea hasara kwa Serikali. 

Pamoja na Haya Mliosema Viongozi Wetu sisi kama Wananchi Tunakiri Tumekosea  kutumia Bandari zisizo  rasmi, Tatizo halitokwisha  tunamuomb Mh Rais aone hii changamoto na Atupatie Ufumbuzi  wa haraka haraka, Sio kama Tunapenda kupanda  Majahazi, kwa kweli tunateseka, hakuna Mtu anapemda kuhatarisha Maisha yake lakini kuna dharura zinatubidi tufanye ivyo haziepukiki . 

"Changamoto zinatupata  sisi kama Wananchi  usafiri wa  Kutoka Pemba kwenda Tanga hamna  , Tunaiomba Serikali Itutafutie Mbadala ili kusijitokeze mambo  ambayo sisi hulazimika kuyafanya kutokana na kukosa Mbadala wa usafiri, ambao ni kusaidiwa kuletewa Meli maalum ambayo itasaidia kuchua Abiria wanaotoka Pemba kuelekea Tanga ili Wananchi wasiendelee kutumia Bandari zisizo Rasmi na kuingia hatiani Alisema. "Alisema Hamisa Apolinali  Mwaliandi . 

Kai Khatib kai ambae pia ni Mshirika wa usafiri wa Majahazi  Kutoka Pemba kwenda Mkoani Tanga Alisema kuwa  Kipindi hiki ambacho Usafiri wa Meli  kutoka Tanga kwenda Pemba umekuwa Na usumbufu  na baadhi ya Manahodha ambao hawajulikani kisheria  na Ushirika huo ndio ambao hutumia Mwanya huo kuchukua wananchi na wafanya Biashara  kwa kutumia Bandari zisizo rasmi. 

"Tunatumia bandari Rasmi inayotambulikana kisheria Mambo  yanayofanywa na Baadhi ya manahodha ambao hawatambulikani na ushirika  Ndio hayo ambayo yanajitikeza wanatumia bandari bubu bila sisi kujua". 

Akizungumza na Wasafiri hao waliokamatwa katika Bandari zisizo rasmi ikiwemo Mtambwe, Fundo, hiyo Kaimu wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya  wete Mgeni Khatib Yahya Ambae Pia ni Mkuu wa wilaya ya Micheweni aliwataka wasafiri hao kuacha Mara moja kutumia Usafiri huo  ambao sio rasmi kwa shughuli za kuchukulia Abiria pamoja na kutumia bandari bubu badala yake kutumia bandari Rasmi iliyowekwa na Serikali. 

"Sisi kama Serikali Tunatambua kuwa  siku Rasmi ya  Haya Majahazi hapa katika Bandari ya  wete  Kaskazini Pemba ni Siku ya Jumanne, na Jumapili kuondoma Pemba kuelekea Tanga. 


" Wananchi Napenda Mjue kwamba Usafiri wa Msahua, Majahazi Kutoka Tanga kuja Pemba, na kutoka Tanga kuja Pemba, kubeba Abiria Ni Makosa, Nyinyi abiria ambao Tayari mshafanya hivyo na wananchi mtambue hili, Kuanzia leo  yeyote ambae atakamatwa ni lazima  Sheria ichukue Mkondo wake, kwa Abiria na mnahidha Pia. 

 Aidha  Mgeni Alisema kuwa Serikali ya Wilaya kwa kushirikiana na ...... Haitosita kusitisha safari kwa chombo chochote cha Majahazi ambacho  kitachukua Abiria badala ya Mizigo  na kutumia Bandari Bubu. 

 " Vyombo  hivi havijasajiliwa kwajili ya kuchukulia Abiria  Manahodha mlitambue hili, mnachukua Abiria Mkikamatwa Mjue Tutazuia vyombo  visifanye kazi, tutaviweka pale juu bila Muhali kwa jambo hilo Tunafanya hivyo kwa kuzingatia Usalama wako Wewe Mwananchi . 
Akizungumzia Malalamiko hayo yaliotolewa na Wananchi ambao ni abiria hao waliokamatwa katika Bandari zisizo rasmi Mwenywkiti huyo aliwataka wananchi kuwa waumilivu kutokana na kukosekana kwa Mwli inayifanya safari za Tanga Pemba kwa vile ipo Katika Matengenzo. 
 "Sote tunajua kama meli ambayo ilikuwa inafanya safari za pemba Tanga imeenda Servise ni kwa maslhi yenu wenyenu ingeendelea kutumiwa   inheleta matatizo  Mzigo wa lawama woote ungekuja kwa Serikali muendelee kiwa wastahamilivu alisema. 
 
 Wananchi hao waliokamatwa katika bandari mbalimbali zisizo Rasmi imekuja kufiatia ziara maalum iliyifanywa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Wete kwa kushirikiana na Mamlka ya Bandari wilaya ya wete ZRM  wilaya ya wete pamoja na TRA. 








Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.