TUTAWEKA KIPAUMBELE SEKTA YA ELIMU ZANZIBAR NA KUIMARISHA MASLAHI YA WAALIMU
- Get link
- X
- Other Apps
Na AMINA AHMED MOH’D PEMBA.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi Alisema Serikali yake ina Dhamira Njema ya kuendelea Kuzipatia Ufumbuzi Changamoto Zinazokabili Walimu Unguja na Pemba ikiwemo kuzipatia Ufumbuzi Stahiki zao ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi zao, katika Kuleta Mageuzi ya Elimu Na kuwa katika Mfumo Bora wa Ufundishaji utakaoendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknologia .
Aliyasema Hayo Katika Maadhimisho ya Siku ya Waalimu Duniani yalioambatana n Mkutano Mkuu wa Ufunguzi wa Uchaguzi wa Chama cha Waalimu Zanzibar ZATU uliofanyika Katika Ukumbi Wa ZSSF Tibirinzi Chake Chake Pemba Mapema Leo Asubuhi.
Alisema Chanagamoto mbali mbali ambazo zimewasilishwa na wizara hiyo ikiwemo nyongeza ya Mshahara, Uhaba wa Madarasa , Posho la waalimu, Mafunzo na Ajira Waalimu,pamoja na marekebisho ya Mitaala Serikali imezipatia ufumbuzi kwa Asilimia kubwa hivyo Changamoto zinazoendelea kujitokeza siku hadi siku katika kuimarisha Seketa ya Elimu Zitaendelea kupatiwa ufumbuzi Kwa kushirikiana na Waalimu Serikali na Wadau mbali mbali.
Alisema Dhamira ya Kwanza ni Kuendelea kutafuta vyanzo vya Fedha ambazo zitasaidia kuimarisha Zaidi uchumi wa Nchi ambao utapelekea kuimarisha Maslahi ya waalimu Nchini na kuimarisha Sekta Ya Elimu .
"Serikali Itaweka Kipaumbele katika Bajeti ya Sekta hii ya Elimu kutokana na Mchango wao kwa Taifa ,Pamoja na kutafuta vyanzo vyengine vya Fedha vitakavyosaidia kuimarisha Elimu kwa ununuzi wa Thamani, Vitabu, Ajira kwa waalimu , Pamoja na vitu vyote ambavyo vitasaidia kufundishia, Ni Dhahiri kuwa haja ya kufanya hivyo ni kubwa kwa sekta hii kutokana na ongezeko la Watoto Wetu wanaohitaji kupata Elimu Ambayo ni Haki yao" .
Aidha Aliwataka Waalimu kuona Umuhimu wa kuzitumia Fursa mbali mbali zilizopo za Kujiendeleza kielimu ili kuweza kupata Maarifa Mapya ya kufundishia Wanafunzi kwa Uweledi Zaidi na kuweza kujijengea Heshima Kwa Jamii.
"Fursa za kujiendeleza kielimu hivi sasa zimezidi kuongezeka Nchini Vipo vyuo Vikuu, ambavyo mnaweza Kuvitumia katika Kujiendeleza na Kuongeza Maarifa na kuongeza viwango vyenu vya Elimu."
Hata Hivyo Dk Mwinyi aliwataka Waalimu Kuimarisha Uhusiano Kati yao na Wazazi wa Wanafunzi kwa kuwahimiza kuimarisha Malezi ya Pamoja , kwa watoto ili kuwajengea Maendeleo na Mustakbali Mwema Wa Maisha ya Sasa na ya Baadae.
" Ili watoto waweze kuwa Na Madili Mema Waalimu niwatake kuwa na Mashirikiano na wazazi katika Malezi ili kupata watoto ambao watajiepusha na Tabia hatarishi, na kuwa Raia wema ambao watakuwa Tegemezi katika Maisha ya Baadae" .
Akizungumzia Suala la Uchaguzi wa Viongozi wa Chama Cha Waalimu Zanzibar ZATU Dk Hussein Aliwataka Wanachama wa Chama hicho amabao ni waalimu kuwa Makini katika Kuchagua Viongozi bora watakaofanikisha kusogeza mbele Maendeleo Chama cha Waalimu.
Aidha Alisema kuwa Serikali itaendelea kulifanyia kazi ombi lilitolewa na Waalimu juu ya kupata Tume Maalum ya Utumishi Serikalini kwa Waalimu ambayo itasaidia kuimarisha Maslahi ya Waalimu Nchini.
Awali Akitoa salam za Wizara katika Kilele cha Siku hiyo ya Waalimu Waziri Wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Leila Muhammed Mussa Aliwataka Waalimu Wakuu nchini kusimamia Mitaala Mipya iliyofanyiwa marekebisho kwa Wanafunzi wa Skuli za Msingi.
Aidha aliwaomba waalimu kuendelea kujiunga na Chama hicho ili kukizidishia uhai ambao utasaidia katika kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili waalimu kwa urahisi.
Awali akisoma Risala kwa niaba ya Chama cha Waalimu Zanzibar ZATU Katibu Mkuu wa Chama hicho Haji Juma Omar Alisema kuwa Chama kimeweka Mikakati Endelevu ya Miaka 5 ikiwemo kujadili Maendeleo ya Chama hicho, Kuchagua Viongozi wapya, ambao watahimiza uwajibikaji kwa Waalimu, pamoja na kuunga Mkono juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Nane katika Kukuza maendeleo ya Elimu.
Siku ya Waalimu Duniani huadhimishwa kila ifikapo February 12 Ambapo Vyama vya waalimu kutoka nchi mbali mbali vikishiriki katika Maadhimisho hayo huku Chama cha Walimu Zanzibar ZATU kikiadhimisha siku hiyo kwa kufanya Mkutano Mkuu wa nane ambapo wananchama wa chama hicho Kesho watafanya uchaguzi wa kuwachagua Viongozi wakuu wapya Watakaongoza chama hicho.
Ambapo pamoja Mkutano huo pia Rais wa Zanzibar Alifanya ziara ya Kushtukiza katika Maduka ya vyakula Katika Mji wa Chake Chake Na Machomanne kuulizia Bei ya Bidhaa ya Mchele jumla na reja reja pamoja na kutaka kujua Hali ya upatikanaji wa bidhaa hiyo kutoka kwa wafanya Biashara.
Mwisho.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment