KILIMO CHA MPUNGA MKOMBOZI KWA BAADHI YA WANAWAKE VIJIJINI.

NA - SALMA KHAMIS - UNGUJA 

KILIMO  ni Uti wa Mgongo, huu ni Msemo Maarufu sana ambao hutumika kuhamasisha Kilimo ambacho ni Moja kati ya Nguzo Muhimu kwa Uchumi wa Nchi. 

Sekta ya kilimo ni Miongoni mwa Sekta Tegemazi kwa Wananchi walio wengi hasa Wanawake ambao hutumia fursa ya Kilimo Kujiajiri Wenyewe . 

Visiwani Zanzibar Wanawake wengi wamekuwa wakijishughulisha na Kilimo tofauti  kama mboga mboga ingawa kuna baadhi yao wanajishughulisha na Kilimo cha Mpunga. 

Katika makala hiiii tutazungumzia kuhusu Wanawake wa kijiji cha Mgambo wanavyoendesha maisha yao ya kila siku kwa kutegemea kilimo cha Mpunga. 

Kwa Miaka mingi wanawake wa kijiji hicho kilimo cha mpunga ndio kimekua tegemeo lao katika kuendesha maisha yao. 

Katika kijiji cha mgambo Inaelezwa kuwa wanawake ni kundi  ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa katika kuzalisha zao la mpunga ndani ya kijiji hicho . 

Hali hiyo impelekea wanawake wengi   kuweza kujiajiri wenyewe kwa kulima kilimo   hicho na kuendesha faimilia zao pamoja na kuachana na hali ya utegemezi. 

Wanawake wa kijiji hicho  wameeleza kuwa kilimo hicho kimewapelekea kupunguza gharama za maisha.  
                
"Tunalima sana mpunga kwa muda wa miaka mingi sasa na kilimo hichi kinatusaidia sana kuendesha maisha yetu na Familia zetu, wakati wa Mavuno furaha huongeza katika Familia na kupata wageni kutok maeneo tofauti kuja kufurahia mpunga mpya". 

Aliendelea    " Familia yangu naendesha vizuri sana kupitia kilimo hichi cha mpunga na naweza kuvuna mapolo zaidi ya 8 kwa heka moja tunashkuru riziki zetu tunapata "    Walisema  baadhi ya wakulima 

Lakini tukumbuke kuwa kila kazi haikosi changamoto, kwa upande wa wakulima hao wamedai kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kilimo hicho hali inayopelekea kuwepo kwa uzalishaji mdogo. 


Ukosefu wa Maji ya kumwagilia Mashamba yao  na kutegemea maji ya mvua imekuwa ndio tatizo sugu   kwa wakulima hawo  na kupeleka kuvuna mavuno kidogo na huvuna mara moja tuu kwa mwaka. 

Lakini vile vile wamelalamikia kuwepo kwa ukosefu wa Pembejeo ikiwemo mbolea na dawa  na wanapoipata hupata kidogo tuu ambayo haikidhi mahitaji yao hali inayosababisha kuvuna mavuna yasio na ubora. 

Pia wakulima hawo wameiomba serikali kuwapunguzia bei ya dawa kutoka elfu thelathini (30) kwani bei hiyo  ni kubwa kwao hawaimudu ukilinganisha na maisha yao ni magumu. 

      "Katika kijiji chetu hakuna maji na mpunga unahitaji maji sana ili kunawiri na suala hili tushalipigia kelele sana ila bado hatujajaaaliwa, na pia pmbejeo tunapata kwa shida maana polo moja mnaweza kupewa kwa watu wanne mpaka watano na mtu una heka nzima inakuwa haikidhi na mpunga haustawi na mwisho wake unakufa kwa kushambuliwa na wadudu." 

"Serikali ituangalie pembejeo tuipate na maji watuchimbie visima  ili kilimo chetu kistawi vizuri na kuvuna mavuno mazuri ".
           
     Wamesema wakulima. 

Kutokana na Matokeo ya utafiti uliofanywa na Wizara ya kilimo inaonyesha kuwa uzalishaji wa  zao la mpunga umepungua kutoka tani 40.328 kwa mwaka 2020 hadi tani 30. 353 mwaka 2021  hiyo inaonyesha kuwa nguvu kubwa ya pamoja  inahitajika ili kuimaraisha kilimo cha mpunga Zanzibar. 

Zaidi ya wananchi miatatu(300) katika kijiji cha mgambo wanajishuhulisha na kilimo mbali mbali kama viazi , mihongo, mihindi na mboga mboga na mia moja na hamsini (150)ni wakula wa zao la mpunga. 

Sheha wa shehia ya Mgambo Ali kombo Zubeir amesema zao la mpunga linawanufaisha sana wananchi wake kuendesha maisha yao hasa pale maji , dawa na mbolea zinapopatikana vizur na kwa wakati na Mkulima huvuna zaidi ya gunia nane kwa nusu heka.

Hapo hapo sheha huyo ameiomba mamlaka husika kuwafanyia urahisi wa kupatikana kwa maji ya kumwagilia , dawa na mbolea ili wananchi wake wawez kulima kilimo kilicho bora na kukidhi mahitaji yao.
        "Mimi mwenyew nalima mpunga lakini sasa kulingana na hali ya kutokuwa na maji na pembejeo tunashindwa tuntegemea mvua na mvua mara hiii hamna, sasa kwa kweli mwaka huu ata nusu kilo mpunga haupatikani."
            "Serika ituleteee maji na pembejeo ili kilimo kikubali na kustawi vizur wanachi wapate pesa maisha yao yaweze kunyoooka."
      Amesema sheha.
         
Serikali ya awamu ya nane imeamua kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kuwakomboa wakulima Zanzibar kutoka kilimo duni kisichokuwa na tija na uzalishaji na kuwawekea fursa ya kuwawezesha kupata tija na kuwa na uhakika wa chakula na lishe. 

Katibu mkuu Wizara ya kilimo Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Zanzibar Sefu Shaban Mwinyi amesema kipindi cha kati  kulikua cha changamoto ya pembejeo kutokana na kutolewa kwa upungufu wa gharama Serikali ilikuwa ikitoa asilimia thamanini(80) lakini wananchi walikua wakichangia asilimia ishirini (20) tuu ya gharama ya pembejeo ikiwemo mbegu, mbolea na dawa na hiyo ndio sababu iliokuwa ikipelekea kuleta shida katika ufanisi wa kilimo kwa wakulima.


Akieleza mikakati waliojiwekea Wizara  kuimarisha kilimo hicho  katibu huyo amesema Serikali kwa makusudi imechukuwa jitihada maalum ya kuanzisha mabonde mapya ya umwagiliaji sita (6) yakiwemo matano Unguja ambayo ni bonde la kinyasini, kibokwa, kilombero,chaani na Cheju A na pemba bonde moja la Mlembele hali itakayoleta ufanisi zaidi kwenye ukulima na uzalishaji kwani ukulima wa mpunga kwenye mabonde ya umwagiliaji ufanisi wake ni tofaut  na hulima mara mbili kwa mwaka tofauti  na  kwenye mabonde ya kutegemea Mvua hulima mara moja tu kwa mwaka.

Pia hapo hapo Katibu huyo amesema wameandaaa mafunzo maalum kwa wakulima wa mpunga ili kuhakikisha utaalamu ule unaohitajika wanautumia katika kuendeleza kilimo kilicho bora.
      "Serikali inachukuwa juhudi kubwa sana katika kutafuta namna ya kuwasaidia wakulima ikiwemo kushirikiana na wizara ya kilimo Tanzania Bara  tumekubaliana kufanya kikao hapa hapa Zanzibar na tayari tushafanya lakini hata Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti na baraza la Mapinduzi na yeye hili analisismamia  kikamilifu na ametupa maelekezi tuandae mahitaji yote ya mbolea zinazohitajika na tayari tumemepelekea na saiv anatafuta njia bora ya kulimaliza tatizo hilo."
      Amesema katibu.
  
Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

UHABA WA VITUO VYA POLISI WILAYA YA CHAKE CHAKE BADO MLIMA MREFU KUDHIBITI UHALIFU VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAMU.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.