Kilimo cha Mboga mboga

Na Mwashamba Juma - Idara ya Mawasiliano Unguja 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kilimo cha  mbogamboga na matunda (horticulture) kina mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa Zanzibar pia ni chanzo kikubwa cha ajira na kipato kwa Wazanzibari.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo, kwenye ufunguzi wa kituo cha maarifa cha kilimo cha mbogamboga na matunda, Mpendae Kwabitihamrani Wilaya ya mjini, Unguja.

Alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua mchango mkubwa wa kilimo cha horticulture kwa afya ya Wazanzibari. 

Alisema Zanzibar imeshuhudia ongezeko kubwa la uzalishaji ya mazao ya mboga mboga na matunda kwa mwaka 2021/22, uzalishaji wa mazao ya (horticulture) Zanzibar ulifikia jumla ya tani 148,000 kiasi alichoeleza ni ongezeko la asilimia 68.2 kwa kipindi cha tokea mwaka 2012. 

Alisema ongezeko la uzalishaji limepunguza utegemezi ambapo uagizaji wa matunda na mboga mboga kutoka nje ya nchi umepungua kutoka asilimia 80 tokea mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 26 mwaka 2021. 

Ongezeko hilo alieleza limetengeneza pato la mkulima wa mazao ya bustani kuzalisha na kuuza mazao yake ndani

Aliwahimiza viongozi wa Serikali kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo na taasisi ya TAHA kufanya jitihada za ziada kuhamasisha umuhimu wa ulaji wa mboga mboga na matunda ili kutunza afya.

“Ili tuwe na watu wenye afya njema, hatuna budi kuwa na watu wanaokula mbogamboga na matunda kwa wingi, sehemu kubwa ya watu hawatumii mazao haya kwa wingi” Alisema Dk. Mwinyi

Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kupata elimu sahihi kuhusu uzalishaji, uandaaji wa vyakula vya mboga, matunda na viungo na utumiaji wake ili wapate kujua faida zake na kuimarisha afya zao na kupanua wigo wa soko la mazao hayo. 

Aidha, Rais Mwinyi alieleza Serikali kwa kusirikiana na taasisi ya TAHA itaendelea kukipa kipaumbulee kilimo cha mboga mboga kutokana na umuhimu wake mkubwa kwenye uchumi wanchi.

“Tutaendelea kuzingatia vipaumbele vya kuboresha mazingira wezeshi ya biashara, kuongeza tija ya uzalishaji, kurahisisha upatikanaji wa masoko, kujenga miundombinu ya umwagiliajia na masoko na kuwezesha upatakanaji wa taarifa, utafiti na huduma bora za ugani” Alieleza Dk. Mwinyi

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Ufugaji, Shamata Shaame Khamis, alisema shughuli zinazofanywana taasisi ya TAHA ni utekelezaji bora wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na kuungamkono jitihada za Serikali kwa kuimarisha kilimo.

Alitoa ufafanuzi wa changamoto ya bandarini na uwanja wandege wakati wa mchakato wa usafirishaji bidhaa za mazao ya wakulima, Waziri SHamata alisema tayari Serikali imechukua hatua kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa hatua ya mazungumzo ili kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.

Nae Naibu Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Antony Peter Mavunde alieleza taasisi ya TAHA itawanufaisha sana wakulima wa Wazanzibari na kuwasihi kuzitumia vyema fursa zinazotolewa na kituo hicho.

Alisema Serikali za SMT na SMZ kupitia wizara zao za kilimo wanafanyakazi kwa ushirikianao mkubwa na kubadilisha uzoefu kwenye masuala ya kilimo kwa usatawi wa taasisi zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya TAHA, Mhandisi, Zebadiah Moshi, aliwasihi watendaji wa Shirika la Bandari Zanzibar kutoa kipaumbele cha kusafirisha mazao ya wakulima wa mbogamboga na matunda ili kuwakwamua kimaisha.

Katika hatua nyengine, Mtendaji Mkuu wa taasisi ya TAHA, Jacqueline Mkindi aliziomba taasisi za kiswahili nchini wakiwemo Baraza la Kiswahili Zanzibr (BAKIZA) na Baraza la Kiswahili la Tanzania Bara, (BAKITA) kubuni jina mbadala litakaloondosha ukakasi wa neno iliopo kwenye tasnia hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.