Dimwa Aja na Mikakati Kuimarisha chama cha Mapinduzi.

Na AMINA AHMED MOH’D PEMBA. 
CHAMA cha Mapinduzi CCM Zanzibar Kimesema kitaendeleza   Mazuri yanayofanywa na viongozi Chama Cha Mapinduzi ikiwemo kudumisha Amani, Umoja  Mshikamano , kutetea Maslahi ya Chama, kuongeza idadi ya Wanachama Sambamba na kulinda Muungano  kwa Maslahi ya Wananchi  .

Ahadi hiyo  imetolewa na  Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  Muhammed Said Dimwa Alipokuwa akizungumza na Wananchi, Pamoja na Wanachama wa Chama hicho kisiwani Pemba huko katika ukumbi wa Fidel Castro Wawi Chake Chake  Mara baada ya  Kumalizika kwa Mapokezi  ya aina yake kwa Naibu huyo ikiwa ni Mara ya Kwanza kufika Kisiwani Humo Tangia kuteuliwa kushika Nafasi hiyo. 


 Alisema Dhamira Njema ya Chama hicho  ni kuendelea kuwa Karibu na Wananchi   kwa kuanzisha Darasa la itikadi kwa Ngazi za Matawi  ambalo litasaidia  kuongeza Uelewa na Wanachama Wengi  zaidi  katika Chama hicho ambao watasaidia kuongeza Mashirikiano, kudumisha Amani,na Mshikamano na kupelekea kuongeza Ushindi  Mkubwa Katika Uchaguzi 2025.



 Aidha  Naibu huyo Amewataka wananchama hao kuacha Makundi na badala yake kuweza kuungana Pamoja  katika  kukiimarisha zaidi Chama Cha Mapinduzi, ambacho ni chachu Ya Maendeleo kwa Wazanzibari. 


 Naibu huyo Amewaahidi Wanachama hao kuwa ataendeleza Mashirikiano na viongozi  wa Ngazi zote  ikiwa ni Pamoja na kufuata Ushauri na kupokea maoni ambayo yatasaidia kujenga Uimara wa Chama. 
 Hata Hivyo Dimwa Alisema  Chama Cha Mapinduzi kimedhamiria kuimarisha na kutoa kipaumbele katika Mambo  Mbali mbali ya Maendeleo kwa Akina Mama na Vijana,ikiwemo kuwawezesha Kiuchumi. 

  Awali Akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma Alimpongeza Naibu katibu huyo kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo Zanzibar ambapo alisema kuwa Wanachama wa Chama hicho Kusini Pemba kitaendelea kutoa Mashirikiano katika kuona anakamilisha vyema utekelezaji wa Majukumu yake.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud Amesema kuwa Ujio wa Naibu Huyo kutasaidia kuimarisha Mipango ya Maendeleo ambayo itasaidia kuimarisha Maendeleo kwa Wananchi wa Mkoa huo.


 Wanachama kutoka Matawi Mbali Mbali   Wameshiriki  katika Mapokezi  Ya Kumpokea Naibu katibu Mkuu  Muhammed Said Dimwa   Pamoja na Wajumbe wa Idara  za  Kamati  Maalum ya Nec  ambapo  shamra shamra hizo zilianza Mapema  Leo Asubuhi huko katika  Ofisi kuu za Chama   Chachani Mkoa Kusini  Pemba  zikifuatiwa Na Burudani mbali mbali za Ngoma,  Nyimbo, na Michezo ya kiumbizi kutoka kwa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi. 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.