AKINA MAMA WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA MAENDELEO KUJIKOMBOA KIUCHUMI.
Na RAIFA ABDALLA - UNGUJA.
KATIBU wa Kikundi cha Ushirika Meli Nne Saccos Njuma Ali Muhamed amewataka Wananchi Pamoja na akina mama kujiunga na vikundi vya ujasiriamali, kuweka hakiba na kukopa, ikiwemo , ili kujipatia Elimu pamoja na kuwezeshwa kwenye Shughuli za kujikwamua Kiuchumi ,katika kukuza Maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya Akina Mama Ushirika wa Meli Nne Saccos.
Hayo yameelezwa na katibu wa Meli nne Saccos Njuma Ali ambae pia ni mwanzilishi wa ushirika huo,wakati akizungumza na mwandishi wa habari huko katika afisi za ushirika wa melinne saccos ,Mkoa wa Mjini Magharibi.
Njuma Ali Muhamed - Katibu Meli Nne SaccosAlisema , aliamua kuwakusanya wanawake wenzake katika kuunda ushirika huo baada ya kupata mafunzo ya namna bora ya kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa katika jamii.
“Baada ya kupata mafunzo ya kuanzisha ushirika wa kukopa na kuweka kutoka Umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar, nilirudi kwa sheha wangu na kumshauri, na ndipo tukaanza kukusanya watu ndipo ushirika huu ulipoanza mwaka 2005 ambapo ushirika uliana na wanachama 150” alisema Bi njuma
Alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wanachama wao kabla kupatiwa mikopo wanayoitaka juu ya namna bora ya marejesho, kueka akiba, kuweka amana pamoja na elimu ya ujasiriamali, ambayo itawasaidia kutumia vizuri mkopo wanaopatiwa katika kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
“Kupitia mafunzo wanayoyapata yameweza kuwasaidia wanachama wa ushirika huo kuweza kurejesha mikopo yao mapema, kukuza biashara zao pamoja kutumia vizuri mikopo hiyo katika kufanya shughuli za kimaendeleo” alisema
Aidha alisema kuwa ushirika umefanikiwa kuweza kupata eneo ambalo wamejenga ofisi, maduka pamoja na ukumbi ambao unatumika kwa shughuli mbali mbali za kijamii. Pia wamefanikiwa kuwapatia Ajira vijana 23.
Aliongeza kuwa, mbali na mafanikiyo yaliyopatikana kwa sasa ushirika huo unakabiliwa na Changamoto ya uzorotaji wa marejesho ya mikopo kutoka kwa wanachama jambo ambalo linawarejesha nyuma katika uendeshaji wa kituo hicho, na kuwataka wanachama kuachana na dhana potofu kuwa mikopo wanayopatiwa kuwa haihatajiki kurejeshwa jambo ambalo si sahihi.
Kwa upande wake Khamis Daudi Simba Mkurugenzi idara ya maendeleo ya ushirika alisema kuwa wanautambua vyema ushirika wa Meli nne Saccos na ni miongoni mwa Saccos ambazo zinafanya vizuri Zanzibar.
“Melinne Saccos ni miongoni mwa vyama vya ushirika vya msingi vilivo sajiliwa Rasmi kupitia idara hii, na wanachama wamekuwa wajipatia mikopo na kuweka akiba kwa ajili ya kuendesha maisha ya wanachama. Saccos hii ni namba Moja Zanzibar ambao ina wanachama wengi na wameweza kupata mafanikio mazuri” alisema
Idara imekua ikitoa mashirikiano kwa Saccos zote kwani kupitia suala hili wameweza kuwafikia wanachama wa vyama vya ushirika kwa kueka Afisa ushirika katika ngazi za wilaya, ampabo wamekuwa wakitoa mashirikiano katika kuvisajili, kuvijengea uwezo, kutatua migogoro, kuvilea pamoja na kuvikagua vikundi vyote vya ushirika.
Nae Katibu mtendaji wa mwanvuli wa vyama vya akiba na mikopo Zanzibar (ZASCCU) bwana Abdala Hassan Iddi alisema, ushirika huo umepata Uongozi imara unaongozwa na Bi Njuma kutokana na ubunifu wake ulioambatana ujasiri.
“Ujasiri wake katika kuhakikisha anawakwamua wanawake wenzake kutokana na ugumu wa maisha sio jambo rahisi, kwani ameweza kutoka kwenye mtaji wa shillingi Moja hadi kufikia shillingi bilioni Moja katika ushirika wake. Hivyo naweza kusema kuwa ni super woman” alisema.
Akizungumzia mafanikio aliyoyapata mwanachama wa ushirika huo Iptisam Abadala Salum alisema kupitia elimu aliyopatiwa ameweza kujikwamua na hali ngumu ya maisha, amejenga , anasomesha watoto na ameweza kuajiriwa kwenye ushirika na kuwa muuza duka la bidhaa za Meli nne Saccos.
Nae sheha wa shehia ya Meli nne Nouman Maulid Salum, Alitowa wito kwa wananchi wake kujitokeza kwa wingi kujiunga na ushirika huo Kwani ni miongoni mwa vyama vya ushirika vilivofanikiwa Zanzibar kutokana na maendeleo yake yanayoonekana, na kuepukana na lawama kutoka kwa wanachama wao wanoishi katika shehia hiyo na wanaotoka nje ya shehia hiyo.
Ushirika wa Meli nne saccos ulianzishwa mnamo mwaka 2005 hadi sasa 2023 ambapo ulianza na wanachama 150 kwa sasa una Jumla ya wanachama 1753 wanawake wakiwa ni 1023 na wanaume ni 730.
Comments
Post a Comment