ZOYINA USHIRIKA ULIOFANIKWA KUANZISHA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI WA SABUNI. MADUNGU CHAKE CHAKE CHACHU YA MAENDELEO NA AJIRA KWA VIJANA . WAJASIRIAMALI WALIOWENGI HUCHOTA UJUZI WA KUTENGENEZA BIDHAA KUPITIA MWANZILISHI WAKE WAMEANZISHA VIWANDA KATIKA MAENEO WANAYOISHI.



Na Amina Ahmed Moh’d - Pemba. 

"MDOGO mdogo ndio mwendo " ni usemi maarufu unaohamasisha watu kutimiza malengo waliojiwekea hatua kwa hatua.
 
 Naufananisha msemo  huu baada ya ushirika wa    ZOYINA  kumiliki kiwanda kinachozalisha Sabuni  kwa kutumia miti ya asili ikiwemo mti wa mronge, manjano karafuu  pamoja na liwa ambazo  hutumiwa kwa ajili ya dawa na urembo . 

Kiwanda hicho huzalisha sabuni za maji, sabuni za vipande, Jiki, Scrub   Pamoja na Udi  ambacho kilianza  harakati zake kidogo kidogo kikiwa na mtu mmoja pekee hadi leo hii imekuwa ni  tegemeo la kujipatia kipato kwa vijana zaidi ya 20. 


ZOYINA pia imekuwa ni   moja kati ya vituo vya kujipatia Taaluma  na ujuzi kwa akina mama kutoka maeneo mbali ambao hutumia ujuzi huo katika kujiajiri na kujipatia kipato cha kujikimu na familia zao. 

 ushirika wa ZOYINA ulianza   kuzalisha bidhaa ya sabuni Ya vipande pekee  lakini kwa sasa bidhaa mbali mbali zimekuwa zikizalishwa na ushirika huo. 

  Asili ya Jina la ushika wa  Zoyina limetokana na Herufi za mwanzo za Mwanzilishi ambae mpka sasa ni mwenyekiti wa ushirika huo pamoja na herufi za mwanzo za majina za wasaidizi wa ushirika akiwemo makamo mwenyekiti, katibu pamoja na msaidizi katibu . 

Baadhi ya vijana ambao  kupitia ushirika huo uliofanikiwa kuanzisha kiwanda wanasema  ukombozi waliopata imekuwa chachu ya kujikomboa kiuchumi. 

Omar Issa Omar (29)Mkaazi wa Fueni Chake Chake Anasema kiwanda hicho kimekuwa mkombozi mkubwa katika maisha yake kwa vile sasa amepata sehemu rasmi ya kujipatia kipato  cha kuendesha familia yake. 

"Nilikuwa sina sehemu rasmi  muda wote nashinda maskani, nilishauriwa nijiunge na kikundi cha Zoyina  nashukuru nafanya kazi najipatia riziki   yangu kupitia kiwanda hichi leo, kisingekuwepo sijui ningekuwa mgeni wa nani" . 

" Ujuzi wa  Kutengeneza Jiki ambao leo hii imekuwa ni moja kati ya biashara   zangu zinazonipatia kipato na kuendesha shughuli za maisha yangu na familia yangu  nimeupata kwa Zena Othman  Yahya  alinifundisha mwaka 2013 na  mimi nafundisha na wengine ujuzi ule ule niliopata kwake". 

 Ni maneno ya Fatma  Doto Shauri (47) Mkaazi wa Madungu Chake Chake 

"Kazi yangu kubwa katika kiwanda hichi  ni kupeki sabuni katika vifungashio  baada ya kumaliza  kutengenezwa  inanipatia kipato, hakitoshelezi lakini kinasaidia kupunguza  mahitaji yangu binafsi mimi pamoja na wanaonitegemea ". 

Amini Juma Muhammed ni mfanya biashara za urembo  umri (34) Anasema hufuata Bidhaa katika kiwanda hicho na kuuza mitaani kwa bei ya reja reja na kujipatia kipato cha kuendesha familia yake. 

" Nachukuwa Sabuni za karafuu, Sabuni za Mronge, Scrub pamoja na  Udi  Pale kiwandani  kwa bei ya jumla na mimi narandisha mitaani kwa bei ya reja nanunua na bidhaa nyengine za urembo madukani narandisha  na inanipatia tija siku  Zoyina inanisaidia kwa njia hiyo kiupande wangu. 

 Baadhi ya Vijana ambao  wanaendelea kunufaika kupitia kiwanda hicho ni wale ambao wamepata ajira za muda kufanya shughuli mbali mbali  wanasema  wanatamani  fursa hiyo ingekuwepo kila siku katika maisha yao. 

"Mimi binafsi natamani hichi kiwanda kiwe na uwezo wakutuajiri moja kwa moja isiwe kama hivi   kazi za siku tu  , kwanza mashirikiano  ya bosi wetu  hayakufanyi  uchoke   unafanya roho radhi   Alidai  Hafidh Said 

 "Kwa sasa hii ni ajira yangu ya muda  lakini matumaini yagu ya baadae ni kufanya kazi hapa hapa  kwa sababu najipatia ujuzi kadri ninavyokuja  kufanya kazi huenda nisipopata hapa bhasi nikaanzisha kiwanda changu kwa ujuzi ambao ninazidi kuona hapa" Idrissa Ali Zahor.

 Mafunda Hamad Rubea  Ni sheha wa Shehia ya Madungu anasema kuwa kiwanda hicho kimekuwa mfano katika shehia yake  kwa kuonesha wigo kwa vikundi vyengine lakini pia kutoa msaada  kwa vijana kujipatia kipato. 

" Uongozi wa shehia tunatambua na kuthamini juhudi zilizofikiwa na  kikundi cha Zoyina  na sisi  tunaendelea kutoa mashirikiano  katika kuona kinafikia malengo  iliyoyakusudia. 

Aliendeleza kuwa" Vipo vikundi  ambavyo kutokana na kukosa umakini  vimekosa mkopo vikiendelea kjiimarisha zaidi kufikia fursa hiyo   lakini utayari na  moyo wa kujitolea kufikia maendeleo kwa kiongozi wa kiwanda cha Zoyina Zena Yahya Othman leo hii ni kikundi pekee katika shehia yangu kilichopata mkopo wa pesa nyingi za kuendeleza shuguli za ujasiriamali ni jambo la kujivunia".
 
Moja kati ya vipaumbele  vya Serikali ya Awamu yanane ya Dokta Hussein Ali Mwinyi  ni kuwatambua  rasmi wajasiriamali  kwa kuwapatia vitambulisho maalum, Kuwawezesha kiuchumi kuwapatia elimu ya ujasiriamali, Lakini pia Kuwapatia Mikopo  itayaosaidia kuendeleza shughuli zao   wanazizifanya. 

Tarehe   24/9/2021  katika ukumbi wa  Sheikh Idrissa Abdul wakil Kikajuni Mjini  Unguja Dk  Hussein Ali Mwinyi  Rais  wa Zanzibar Alipokuwa akizindua mfumo wa utolewaji wa vitambulisho  vya wajasiriamali Alitangaza na  kusema kuwa Serikali ya awamu ya nane imekwisha tenga  Jumla ya  shilingi Bilioni 50  pamoja na kufanya mazungumzo na mabenki mbali mbali  nakuwa tayari kuongeza Bilioni 50   kwa ajili ya kupatiwa mikopo kwa wajasiriamali  wadogo  wadogo Unguja na Pemba. 

"Nimeanza kufanya mazungumzo na taasisi za fedha kwa lengo la kutafuta njia bora za kushirikiana  na kutafuta namna bora ya kutoa mikopo   hiyo kwa  wananchi na bahati Nzuri benki ya CRDB imeonesha hamu kubwa ya kutaka  kushirikiana na serikali katika kufanikisha utoaji wa mikopo hiyo". 

Waswahili wanasema  " Kuvuja kwa pakacha Ni Neema kwa Mchukuzi  Ndivyo ninavyofananisha msemo huu    Ushirika wa  Zoyina kupata  Neema  iliyotangazwa  na Rais wa Zanzibar Dk Hussein  Siku ya  tarehe 24 huko Kikwajuni  lakini pia Maeneo mbali mbali   alimokuwa akigusia suala hili. 

  Zena Othman Yahya  ni Mwenyekiti  na Mwanzilishi wa  ushirika wa Zoyina cooperative  ambapo anasema  Haikuwa kazi rahisi kufika hapo alipo sasa katika kukuza  ushirika huo  hadi kumiliki kiwanda ambacho ni fursa ya vijana kujipatia kipato, Kuwa ushirika darasa kwa wajasiriamali lakini pia Kupata mkopo wa Serikali.

Kitu pekee kilichonifikisha hapa ni moyo wa kutokata tamaa  subra pia, vikwazo ni vingi lakini nilisimama  sikuchokaniliamini ninaweza na kweli  leo hii nimekuwa tegemeo na mkombozi kwa waliowengi ". 

 
" Kiukweli nilianza mbali mwaka 2003 nikiwa peke yangu nilianza kwa mtaji wangu mwenyewe  kutengenza scrub kupitia miti asili,  niliona kuna  haja kutafuta elimu zaidi  kutengeneza  izi bidhaa na nikamtafuta baba mmoja mkaazi wa wete ambae alikuwa anafanya kazi  ushirika wa viwanda vidogo alikuwa anakuja nyumbani kwangu kunifundisha na mimi nilkuwa namlipa,nilibaini kuna fursa za kujikwamua  naweza kutengeneza nikapata kipato nikafanya hivyo". 

"Niliendelea kidogo kidogo  mwaka 2008 nikaanza kuunda kikundi  baada ya kuona shughuli zimekuwa nyingi  nikiwa sina msaidizi  kilianza watu  40  wanawake 34 wanaume 6  kukosa moyo wa kujitolea kulipelekea kuondoka mmoja mmoja siku hadi siku mpka kubakia watu saba wanaume 6 na mimi pekee tunaendelea vyema mafanikio yanaendelea kuoatikana  mpka leo hii tunashukuru. 

"Jambo la kushukuru waliondoka wote waliondoka wakiwa tayari wanaujuzi wakutosha katika  utengenezaji wa vitu mbali mbali na waliowengi wanaendelea kutumia ujuzi huo".

   
  Mwenyekiti wa Ushirika wa Zoyina -  Zena Yahya Othman.

 "Nimetoa elimu ya vitendo katika taasisi mbali mbali za elimu hapa pemba ikiwemo Skuli ya Msingi Madungu  jinsi  ya kutengeza sabuni,  Chuo Cha ufundi  Rans   nimevifikia vikundi mbali mbali  kutoa elimu hii na humo mote ilikiwa nakusanya wanawake  zaidi ya 40 darasa moja kuwapatia ujuzi huu Wapo walikuwa wakinipigia simu kunishukuru baada ya kuanzisha shughuli zao".

Licha ya Mafanikio hayo lakini pia Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa changamoto inayowakabili ni ukosefu wa soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao wanazozizalisha ambapo kupitia makala hii akaiomba Serikali pamoja na wafadhili mbali mbali kusaidia kulioatia ufumbuzi suala hilo. 

MATUMAINI YA BAADAE.
 
 Hata Hivyo  Zena alieleza mipango ya baadae ya ushirika wa Zoyina ni kutoa fursa za ajira za kudumu katika kiwanda hicho kwa  watu 8, kuzalisha uzalishaji zaidi kutoka michi 5000 hadi kufikia 10000 pamoja na kutoa ajira zisizo rasmi 100  kwa vijana. 

" kwa sasa ajira zisizo rasmi  ni 25 vijana wanakuja wala wanapeki wale wanasambaza mitaani malipo ya siku lakini malengo ya baadae ni kupata vijana hawa 100 watakaofanya kazi hizi, ushirika una wafanya kazi   6 ambao wa najipatia mshahara kwa mwezi malengo ya baadae ni kuongeza tena Wafana kazi 8 amabao watapa ajira za kudumu haoa katika kiwanda hichi".

 Hivi karibuni Kiwanda  hicho kimepata  bahati ya Kupata Mkopo Wa Enuka kiuchumi wa Shilingi Milioni 25  Unaoendelea kutolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa wajasiramali ambao lengo lake ni kuwezesha wajasiriamali ambapo Zena anasema 

" Mkopo wa benki nimepata bila usumbufu wowote kwa sababu nilikuwa na vielelezo vyote muhimu  vya kuaminika   , wengine wamekosa fursa hii kutokana na kukosa vile vitu muhimu benki wanavyovihitaji kama  vithibitisho vya kupatiwa mkopo kama wajasiriamali unaodelea  kutolewa na Rais kwa wajasiriamali "

" Mkopo umeniongezea  kasi ya utendaji awali tulikuwa tunazaisha lakini kwa mikono na mashine ambayo ilikuwa inazalisha kwa wingi michi 100 lakini Mkopo umesababisha kupata mashine ambayo inazalisha michi 5000, tunaagiza malighafi  kwa wingi ukilinganisha na awali, tumepata ofisi yetu wenyewe jambo ambalo awali tulikuwa tunalipia kodi kupitia mkopo.

Ni maneno ya Zena hayo Mweyekiti wa Zoyina Cooperative. 
  Issa Othman Muhammed ni mume wa Mwenyekiti wa Zoyina anasema Ushirika huo unaosimamiwa na mke wake umekuwa msaada mkubwa  katika familia yao katika kukidhi mahitaji na matumizi ya familia. 

 Baadhi ya   wananchi ambao wanatumia Bidhaa za sabuni ya Mronge,  Karafuu, n Manjano  pamoja Scrub zinazozalishwa na kiwanda hicho wamezungumza na  mwandishi wa Makala hizi ambapo wamesema  Sabuni hizo  zimekuwa tiba na zinaendelea kutunza urembo wa ngozi na miili yao.

"  Hivi karibuni mwanagu  alifanya Pele za  Tete nikawa  na mpka mara kwa mara  povu la sabuni ya Mronge wiki tu zilififia hzikurudi tena ". Fatma Salum Sefu maarufu Mama duli  mkaazi wa karibu na kiwanda hicho cha Zoyina kilichopo Madungu Mwanamashungi Chake Chake.

" Sabuni Ya karafuu inanifaa sana uso wangu umekuwa hauna mafuta tangu nimeanza kutumia sabuni hii na natumia kila siku  kusafishia uso Kauthar Hakim   (21).


Mimi natumia kwa mda sasa inansaidia    kuondoa  mmba kwenye ngozi yangu umepungua kwa kaisi kikubwa ukilinganisha na awali nilivyokuwa 
Alisema  Baba  Is-haka  ambae jina lake kamili hakutaka liandikwe katika makala hii. 

Jukumu la Uwakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi ni kutoa taaluma  ya uzalishaji, Mtaji kwa wananchi, wajasiriamali wa vikundi, binafsi, pamoja na wawekezaji wazawa uzalishaji wa bidhaa zenye ubora masoko, ushawishi wa uwekaji miundo mbinu   pamoja na kuboresha uzalishaji kwa mbinu za kisada. 

Mratibu wa  Wakala  wa Mifuko ya  Uwezeshaji wananchi kiuchumi Pemba   Haji Khamis Haji  anasema uwakala huo  unaendelea na shughuli za uwezeshaji kwa wajasirimali wa aina mbali mbali ambapo wa wanawake pekee  wametengewa  asilimia 35  ya fedha  zote zilizotolewa sawa na shilingi bilioni 280 kati  fedha zilizotolewa kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kupata mkopo. 

 Sheria ya wakala wa  uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar mwaka  2022  katika ukurasa wa 14  haikuwaacha nyuma  wajasiriamali wanawake katika makundi mabli mbali  ambapo imeweka na kutaja wazi  makundi ya wajasirimali wanawake  wanayo haki ya kupata fursa ya kuwezeshwa kiuchumi kwa kupatiwa  taaluma, mitaji pamoja na kujengewa uwezo na mazingira rafiki  ya kuendesha shughuli wanazofanya. 

Mwisho


  

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.