Wakandarasi Miradi ya elimu Pemba wapewa onyo.
Na Fatma Suleiman
Katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Khamis Abdulla Saidi amesema hatamvumilia mkandarasi yoyote ambae atakwenda kinyume na makubaliano ya mikataba .
Katibu Ameyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea miradi ya ahueni ya UVIKO 19 inayotarajiwa kukabidhiwa hivi karibu.
Amesema kua watachukua hatua za kisheria kulingana na mikataba Ili kuhakikisha Kila mmoja anafanya wajibu wake.
Aidha amesema wamekua wakitumia jitihada kubwa za kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo hivyo kwa yoyote atakaekwenda kinyume hatua za kisheropia zitachukuliwa.
Kwa upande wake Afisa Mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya amali Mwalimu Mohd Nassor Salim amesema, kama wizara wameamua kufuatilia miradi kwa karibu Ili kuipata kwa wakati ulio kusudiwa.
Aidha amesema kuwa malengo ya wizara ni kuhakikisha miradi hiyo ifikapo January iweze kutumika kwa wanafunzi kujisomea.
Nae Mhandisi Wzara ya Elimu khamis Rashid Mtara amesema kuwa licha ya ujenzi kuendelea vizuri lakini Bado kuna wakandarasi wengine hawakuwajibika kama ilivyotakiwa .
Comments
Post a Comment