SHIJUWAZA Yatoa msaada kwa watu wenye ulemavu Pemba.
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D
Jumla ya Familia saba za watu wenye ulemavu pamoja na mazingira magumu zimepatiwa Msaada wa Chakula ikiwemo Unga Sukari na Mchele kutoka Shirikisho la jumuia za watu wenye ulemavu Zanzibar Shujiwaza.
Akizungumza katika ziara maalum ya kuzitembelea familia hizo katika familia maeneo mbali mbali kisiwani Pemba ikiwa ni shamra shamra za kuelekea siku ya watu ulemavu duniani Mwenyekiti wa Shirikisho la Jumuia ya watu wenye ulemavu Mwadawa Khamis Muhamed Aliwataka wasimamizi wa familia hizo kujiunga na jumuia za watu wenye ulemavu ili kuweza kupata haki zao mbali mbali.
Amesema watu wengi wenye mahitaji maalum wamekuwa wakipata haki zao muhimu baada ya kujiunga katika vyama na jumuia mbali mbali na kubadisha maisha yao kiuchumi.
Tumeamua kufanya ziara hii ambayo ni maalum kuwatembela watu wenye ulemavu kuwafariji lakini pia kuwatia moyo kuona kama hawako eke yao tinawajali na kuwathamini niwaombe wasimamizi kuona umuhimu wa kuwasajili katika jumuia mbali mbali ili kupata fursa watakapokaa ndani tu hazitowafikia.
Ali Hassan Ali Afisa kutoka baraza la watu wenye ulemavu Zanzibar kutoka wilaya ya Micheweni Amesema Baraza hilo litaendelea kutoa mashirikiano kwa jumuia zinazoendelea kusaidia watu wenye ulemavu kwa katika kushirikiana kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili watu hao.
Baraza kama serikali tutaendelea kutoa mashirikiano ikiwa ni pamoja na kusaidiana na jumuia mbali mbali kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ukemavu tutaendelea kushirikiana kuwapatia mahitaji yao muhimu ikiwemo visaidizi mwendo.
Nae Kwa upande wake Afisa Mtendaji Kutoka Shirikisho la jumuia za watu wenye ulemavu Pemba Aisha Abdalla Juma Aliwataka wazazi na walezi Kisiwani humo kutoa mashirikiano katika kutetea haki za watu wenye ulemavu sambamba na kuacha ubaguzi katika malezi na uahirikishwaji katika mambo ya maendeleo.
Kila mtu Anapaswa kutoa mashirikiano kwa watu wenye ulemavu kusimamia kupata haki zao ikiwemo haki hii ya kutambulika hivyo tunawajibu wakuwashirikisha katika mambo ya maendeleo ambayo wanayafanya.
Wakizungumza baadhi ya Wanafamilia hao waliopatiwa msaada huo na shirikisho la jumuia za watu wenye ulemavu wameshukuru kitendo hicho walichofanyiwa ambapo wameziomba taasisi na jumuia nyengine kuiga mfano huo wa shirikisho kuwasaidia na kuwatatulia changamoto zao zinazowakabili.
Tumepokea msaada huu kwa furaha sana kwani ni wachache wenye mioyo ya kusaidia tunawaomba na wengine waige mfano huu kutusaidia changamoto nyengine ikiwemo sehwmu za kukaa na kufanya shughuli zetu.
Alisema Time Ramadhan juma mtu mwenye ulemavu Micheweni majenzi amabae pia ni mjasiramali wa ushoni.
Msaada huo umetolewa katika Eneo la Inga ndugu Mvumoni , Mbuzini, Chake Chake, Sizini, Mibrani konde, Pamoja na Micheweni kwa haji shehia ya Majenzi.
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment