E Goverment yasema haya kwa mawakala wa mtandao.

Amina Ahmed Moh’d. 

Mkurugenzi Mtendaji  Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar Said Seif Said    Amewataka  watoa   huduma wanaotumia manunuzi kupitia mfumo  wa mtandao  (E - PROCUREMENT)  ambao hawajajisajili rasmi kuitumia fursa ya kujisajili   ili kupata fursa  ya   kushiriki katika ushindani wa kupata zabuni  na ununuzi wa vitu  vya serikali.
Ametoa wito huo Alipokuwa akizungumza na watoa huduma kutoka maeneo mbali mbali kisiwani pemba katika mkutano maalum wa kusikiliza  maoni ya watumiaji wa  mfumo huo   uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango  Gombani Chake Chake pemba  mapema Leo Asubuhi.

 Amesema  Lengo  ni kuweka uwazi katika utumiaji wa mifumo  na utowaji wa zabuni na ununuzi wa vitu vyote vya  Serikali  jambo ambalo awali halikuwepo  kutokana na kukosekana kwa mfumo huo.


Aidha Mkurugenzi huyo  Amesema kuwa  mamlaka hiyo itaharakisha kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizotolewa na Watoa huduma hao ili kuwaondoshea usumbufu na kasoro ndogo ndogo   zinazowapa usumbufu katika utumiaji wa  mfumo huo.


Mkutano huo  wa siku  moja kwa watoa huduma  wanaotumia  manunuzi  ya vitu vya serikali  kupitia mfumo mtandao umejadili mambo mbali mbali  ambayo yatasaidia kuboresha mambo mbali mbali katika mfumo huo ambapo watoa huduma wa vitu mbali mbali     ikiwemo  vifaa vya magari,  vifaa vya ofisini, pamoja na watoa huduma za vyakula  washiriki na kutoa maoni yao katika mkutano huo ambaoo awali waliiomba mamlka hiyo kuwapunguza  makato  pamoja na kuweka uwazi katika vitu mbali mbali vinavyofanyiwa manunuzi.

Mwisho 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.