Wamiliki wa Vyombo vya habari vya Mtanadao fuateni sheria za habari.
Na AMINA AHMED MOH’D
Wamiliki wa Tv radio na magazeti ya mitandao Kisiwani pemba Wametakiwa kutokiuka sheria zilizowekwa na tume ya utangazji Zanzibar katika kutumia mitandao hiyo kufanya kazi za kihabari.
Akizungumza na wamiliki wa vyombo hivyo katika ukumbi wa Wizara ya Habari Gombani Chake Chake katika mkutano maalum wa kutoa elimu juu ya matumizi sahihi Ya Matumizi na uwekeji wa maudhui za kihabari mitandaoni Katibu Mtendaji Tume Ya utangazaji Zanzibar Sleiman Abdalla Salum Alisema Baadhi Ya Wamiliki wamekuwa wakikiuka sheria za habari n kuweka maudhui ambazo hazina maadili.
Alisema kufanya hivyo Ni makosa hivyo ni vyema wamiliki hao kitumia vyema mitandao ya kijamii kwa kufuata sheria miko na maadili ya habari ili kuepuka kuingia katika matatizo.
" kumekuwa na baadhi ya vyombo vya mitandaoni vinafanya vile vinavyojiskia hakuna maadili katika uwekaji wa maudhui, hawazingatii sheria za uandishi wa habari wanafanya vile tu wanavyojiskia wao.
" Hii tabia inaweza kupelekea wamiliki wakaingia mtatizoni ni vyema mkatumia maadili kufuata sheria pia.
Aidha Sleiman aliwataka wamiliki ambao si waandishi wa habari kushirikiana na waandishi wanapofanya kazi zao za habari ili kuepuka kuingia katika matatizo
"Wapo wale ambao wanamiliki kamera microphone wanamiliki youtube acount wanaamua kuingia mitaani kuhiji watu bila kujua ABC kuhusu habari wanatuma kwenye mitandao hii sio sahihi Wenye tabi hiyo wanatakiwa waiwache mara moja au washirikiane na wanaojua endapo watahitaji taarifa mfuate sheria hata kuwafuata wanaojua taaluma hiyo kuwaelekeza.
Kwa upande wake ofisa mdhamini wizara y habari Pemba MFamau Lali Mfamau Aliwataka wamiliki hao kuweka mipaka katika uwekaji maudhui kwa kufuata sheria za habari mitandaoni.
"Hakuna Uhuru usio na mipaka Mtumie mitandao kwa sheria zilizowekwa fuateni taratibu za kihabari habari zinataratibu zake msikiuke.
Kwa Upande wake Mrajis Tume ya utangazaji Zanzibar Sheikha Haji Dau aliwataka wamiliki hao kusaijili vyombo vyao ili kuweza kufanya kazi kwa kutambulikana kwa mujibu wa sheria ili kuepuka usumbufu wa kutokufungiwa vyombo vyao.
Mwisho
Comments
Post a Comment