Wajasiriamali kilimo ca mboga mboga Wamemshukuru Rais wa Zanzibar.

Amina Ahmed Moh’d 

Mkuu wa wilaya ya Wete Mkoa wa kasakazini pemba amewataka wananchi na wajasiriamali   kuzitumia fursa za kujikomboa  kiuchumi zilizotolewa Na Rais wa Zanzibar  Ikiwemo Mikopo Ya wajasiriamali na kuwekeza katika kilimo. 

Aliyasema Hayo Alipokuwa  Akizungumza na wananchi wa vijiji vya pujini  Mara baada  kumaliza  ghafla ya kukagua na kushiriki zoezi la uvunaji wa   Zao la tungule katika shamba la wajasiriamali wa mboga mboga  wa kikundi cha Mshikamano Lililopo Kijili Pujini wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba ikiwa ni shamra shamra za kutimiza Miaka miwili Ya uongozi Wa Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi .

Alisema   Serikali  imeweka mazingira ya kuimarisha uchumi na kuwa endelevu  kwa wananchi  ambao utawasaidia kujikomboa kiuchumi na kuweza kujiajiri  kwa kuwawezesha  na kuwapatia Mikopo  hivyo ni vyema kuitumia fursa hiyo kwa shughuli mbali mbali ikiwemo kilimo.

Aidha Mkuu wa wilaya Huyo ameitaka wizara ya kilimo  umwagiliaji maliasili na mifugo  kushirikina na wizara ya Maji ili  kusaidia upatikanaji wa maji katika mashamba ya wajasiriamali wa kilimo  cha mboga mboga Kijili. 

"Wizara ya kilimo  Mzidishe jitihada  kuwa karibu na wizara ya maji  ili yasipopatikana maji ya bomba katika shamba  bhasi waweze kuwasaidia mbinu za uongezaji wa visima krqhisisha upatikanaji wa hiduma za maji". 

Katika Hatua nyengine Mkuu huyo Aliwataka wananchi wa Pujini kujiepusha na vitendo vya udhalilishaji sambamba na kudai risiti wanaponunua bidhaa  mbali mbali ili kusaidia upatikanaji wa kodi katika biashara mbali mbali.

Akizungumza  kwa niaba ya ofisa  mdhamini wizara ya kilimo umwagiliaji maliasili na mifugo   Mkuu wa idara ya kilimo  Pemba  Asha Omar Faki  Alisema juhudi zilizofanywa na rais huyo kwa  kutoa mikopo ya  fedha  za ahuweni ya uviko 19  kwa  wajasiriamali  wa kilimo  cha mboga mboga  na matunda zimeleta mafanikio   katika shughuli za kilimo  kwa wakulima hao. 

"Kupitia fedha za covid 19 wajasiriamali hawa  wameweza kupata mafanikio ikiwemo  kuzalisha maji, pamoja na pembejeo jambo ambalo limekuwa, sote tunaelewa kuwa kilimo bila maji haiwezekani kupitia mkopo huu umewasaidia wao kuchimba kisima, kuweka miundo mbinu ya maji na kuweza kumwagilia kwa matone ambazo ni teknolgia bora za kisasa na pia wameweza kupata pembejeo za kilimo kupitia fedha hizo wameweza kufanikisha. 

Aidha  Alisema kuwa  wizara itendelea kushirikianana wakulima mbali mbali ambao wameamua kujikomboa kupitia shughuli za kilimo. 


Awali Akizungumza kwa niaba ya wajasiriamali wa kilimo cha mboga mboga  kikundi cha Mshikamano  Kijili Pujini Mwakilishi wa kikudi hicho Abassi Hassani  Issa  wamemshukuru Rais wa Zanzibar  kwa kuwapatia fursa za mitaji  wananchi wa pujini kupitia kikundi hicho na  kuwa  wanufaika  wa fedha za ahuweni ya  uviko mkopo ambao una masharti nafuu  ambao tunanufaika nao . 

" Kupitia shamra shamra hizi za kutimiza miaka miwili Tunakushukuru Dk Mwinyi  sisi wajasiriamali wa mboga mboga pujini kwa kutupatia fursa za mitaji kupitia programu  ya Enuka  tunaona jitihada zako  katika kupunguza tatizo la ajira na utegemezi na kupunguza umaskini  kwetu sisi wananchi wako ". 

  Tunaimani na uongozi wako   tunaamini ahadi zako   ulizotuahidi katika kipindi cha kampeni kutupatia mikopo ambayo leo hii imeanza kutukomboa n kuttengenezea ajira sisi vijana. 

 Aidha Mwakilishi wa kikundi hicho Alisema Kupitia kilimo hicho kilichoanzishwa kupitia fedha za mkopo huo tayari kimezalisha ajira zaidi ya 100 ambazo wananchi hunufaika na kujipatia kipato  kupitia kilimo hicho.

  "Mshikamano Tumezalisha ajira Zisizo rasmi   miamoja   kupiti kilimo watu wananufaika kwa  kilimo hichi kuna wakulima , wanaovuna, wanaopalia shamba, walinzi kupitia  ahadi zako  za kutengeneza ajira leo hii tumeweza kuzalisha ajira hizo. 
    Hata Hivyo Mwakilishi huyo ameiomba serikali kupitia wizara ya biashara  kuwasadia kutatua changamoto ya soko la uhakika la kuuza bidhaa zao wanazozizalisha   ili kufikia zaidi lengo liliowekwa na rais wa Zanzibar  kujikwamua kiuchumi.

"Pamoja na yite hayo bado kilio chetu Wajasiriamali wa kilimo cha mboga mboga na matunda hatuna soko la uhakika ambalo litasaidia kuuza biashara zetu baada ya mavuno jambo ambalo linaturudisha nyuma  zaidi kuona mazao yanakosa wateja tunaomba serikali itusaidie kupata ufumbuzi wa tatizo hili".

   wajasiriamali wa kilimo cha mboga mboga Kijili Pujini ni miongoni mwa walionufaika na  mkopo wa shilingi milioni Tano  na kuanzisha shughuli ya kilimo cha mboga mboga  kujikwamua na umaaskini ambapo Mkutano huo wa kumshukiru rais huyo  ni katika   kusherehekea kutimia miaka miwili ya uongozi  umehudhuriwa naa viongozi mbali mbali kisiwani pemba ikiwa ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya  Chake Chake, Mkoani, Maofisa wadhamini wizara mbali mbali pemba viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Pamoja na Maafisa kutoka wizara ya kilimo. 
Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.