Taasisi Ya kusafirisha mahujaji Arafat Haji na umrat Services Yawatoa hofu.

NA-  AMINA AHMED MOH’D 

TAASISI YA KIDINI  ya Arafat  Haji na  Umrat Services imewatoa hofu  waumini wa dini ya kiislam  Nchini  wanaotarajia kwenda katika miji mitukufu  Makka Na Madina  kutekeleza ibada ya hijja  Mwaka 2023 sawa na mwaka 1442 Juu  suala la uzoefu wa kufanya harakati za kusafirisha mahujaji.
Alitoa Kauli hiyo  Mwenyekiti Wa Taasisi Ya Arafat haji na umrat  Services  Sheikh Khalifa Abdalla   Said  Mapema  leo asubuhi  Alipokuwa akizungumza na na kujibu maswali yalioulizwa na baadhi ya  waumini wa dini ya kiislam kutoka maeneo mbali mbali ya kisiwa cha pemba waliofika katika kongamano Maalum la uzinduzi wa taasisi hiyo  huko  Samail Gombani Chake Chake.

 Alisema  uzoefu na uaminifu walionao viongozi na wasimamizi wa taasisi  hiyo   katika kusimamia  safari za  za mahujaji ni wa muda mrefu licha ya kuwa mpya kwa taasisi hiyo .

"Wasimamizi wa taasisi hii tuna uzoefu mkubwa  tumesimamia suala hili katika taasisi nyengine   takriban sote mnaotuona  hapa mbele yenu  katika kusimamia na kuongoza jambo hili. 

Awali akizindua taasisi hiyo Sheikh   Khamis Salum Ali  Aliwataka Wasimamizi wa  hao  kubeba  jukumu hilo kwa kutumia hekima na busara ili kufanikisha malengo yaliokusidiwa na mahujaji  kwa kutekeleza majukumu ya uongozi kikamikifu. 

" Mtekeleze Dhima hii   kubwa  kusimamia  kutekeleza ibada ya hijja  kwa waumini  bila kujali  maslahi ya kidunia . 


Kwa upande wake  Sheik Khamis Kassim Haji kutoka taasisi hiyo  Aliwataka waumini hao waliofika katika kongamano  hilo kuweka  nia ya kufanya ibada ya hija na kuwa mabalozi kwa wengine  juu ya Taasisi hiyo. 

"Hija sio fedha  bali ni taufik ya Allah  hivyo  ni vyema kila mmija wetu kuweka nia il kuliafikisha jambo hilo kwa pamoja"

Nae  katibu  wa Jumuia Ya Arafat haji na umrat Services Sheikh Sleiman  Ahmed  Moh’d   Alieleza  kuwa  

Lengo la kuanzishwa  taasisi hiyo ya kusafirisha  mahujaji nchini ni kusaidia  Waumini wa  dini ya kiislam kutekeleza ibada  ya hija bila usumbufu wowote . 

Taasisi Ya Arafat haji na umrat Services  ni Taasisi ya kidini ambayo imezinduliwa ramsi leo yenye   lengo la   kusafirisha  mahujaji wa Kisiwani Pemba Unguja na Dar essalam , pamoja  na kufanya harakati mbali mbali za dini  ikiwemo kusaidia  mayatima wajane na watu wasijiweza.


Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.