Serikali Ya Mapinduzi ya Zanzibar Yasema Haya.

NA FATMA SLEIMAN ABRAHMAN 


Serekali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia raisi wake Dk Hussein Ali mwinyi imesema imedhamiria kuwaekea miundombinu Bora wananchi wake katika kuona wanaboreshea maisha Ili kua na  maendeleo endelevu kwa wote .

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor masoud katika Kijiji Cha mleteni wilaya ya wete  ikiwa ni miongoni mwa mwendelezo wa shamra shamra Uongozi wa kutimia miaka miwili ya Dk Hussein Ali Mwinyi wakati alipokua akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho.
 Amesema  kua lengo la raisi ni kuwaboreshea  wananchi wote katika kujiajiri na kujiingizia kipato hivyo ni wajib wa Kila mmoja kuendelea kutunza miundombinu ambayo inaletwa kwa ajili ya maslahi Yao .

Nae Mkuu wa Wilaya ya micheweni  Mgeni Khatib Yahya amesema kua Kijiji Cha mleteni kilikua Kiko nyuma kimaendeleo lakini kupitia juhudi za raisi kwa sasa kimeweza kufikiwa na neema hizo 
Akiwasilisha taarifa ya kitaalamu meneja wa shirika la umeme tawi la Pemba  amwashukuru wananchi wa mleteni kwa ushirikiano wa dhati walioutoa kwao wa kuendelea kujiunga na huduma hio ya umeme . 

Nao wananchi wa vijiji hivyo wameishukuru serekali ya mapinduzi kwa kuwapelekea huduma stahiki katika makaazi Yao kwani imekua ni mkombozi  na kuwaomdolea  kilio kikubwa ambacho walichokua nacho hapo awali .
Vijiji vya mtakuja mikinduni na mgelele vilivyopo  wilaya ya wete ni miongoni mwa vijiji vilivyopelekewa huda ya maji , Barbara ,umeme na kujengewa skuli kutokana na umbali mrefu uliokuepo wa kuzitafuta huduma hizo  ambapo kina kaya zaidi ya 35.


Comments

Popular posts from this blog

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

UHABA WA VITUO VYA POLISI WILAYA YA CHAKE CHAKE BADO MLIMA MREFU KUDHIBITI UHALIFU VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAMU.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.