Madereva wapewa onyo

NA OMAR HASSAM - UNGUJA

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amewataka madereva wa gari za kubebea watalii kujiepusha na matukio ya uhalifu dhidi ya watalii na badala yake watii sheria za nchi ili watalii wanaokuja nchini wawe salama.
Akizungumza na madereva wa gari zinazobebe watalii huko hoteli ya amani alipokua akisikiliza kero za madereva hao amesema madereva wasitumie vibaya fursa ya kusimamishwa katika vituo vitatu  vya jozani, mwera na mahonda kufanya uhalifu. 
Amesema bado utaratibu wa kutumika kwa vituo hivyo utaendelea lakini lakini Askari watawasimamisha pahala popote ikiwa gari hizo zitatiliwa mashaka ya kufanya uhalifu au kukiuka sheria za usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi wa Polisi Richard Tadei Mchomvu amesema wamezikamata gari mbili Z 761 gt aina ya Noah na Z  856 MM Alphard za kubebea watalii ambazo zimehusika katika matukio ya unyanganyi wa watalii na kubebea mali za wizi.
Kwa upande wake Mratibu wa Kikosi cha Polisi Utalii na Diplomasia kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar Amour Mtumwa Ali ameeleza kuwa gari nyingi za kubebea watalii hazijajiunga kwenye kampuni yanayotoa huduma za watalii hali inayokosesha mapato kwa serikali.
Kwa upande wao madreva hao wamesema wamekuwa wakisimamishwa mara kwa mara na askari hali inayotoa usumbufu kwa madereva na wageni wanaowabeba.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.