Dk Mwinyi Na Maendeleo endelevu
NA FATMA SLEIMAN ABRAHMAN
Serekali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia raisi wake Dk Hussein Ali mwinyi imesema imedhamiria kuwaekea miundombinu Bora wananchi wake katika kuona wanaboreshea maisha Ili kua na maendeleo endelevu kwa wote .
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor masoud katika Kijiji Cha mleteni wilaya ya wete ikiwa ni miongoni mwa mwendelezo wa shamra shamra Uongozi wa kutimia miaka miwili ya Dk Hussein Ali Mwinyi wakati alipokua akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho.
Amesema kua lengo la raisi ni kuwaboreshea wananchi wote katika kujiajiri na kujiingizia kipato hivyo ni wajib wa Kila mmoja kuendelea kutunza miundombinu ambayo inaletwa kwa ajili ya maslahi Yao .
Nae Mkuu wa Wilaya ya micheweni Mgeni Khatib Yahya amesema kua Kijiji Cha mleteni kilikua Kiko nyuma kimaendeleo lakini kupitia juhudi za raisi kwa sasa kimeweza kufikiwa na neema hizo
Akiwasilisha taarifa ya kitaalamu meneja wa shirika la umeme tawi la Pemba amwashukuru wananchi wa mleteni kwa ushirikiano wa dhati walioutoa kwao wa kuendelea kujiunga na huduma hio ya umeme .
Nao wananchi wa vijiji hivyo wameishukuru serekali ya mapinduzi kwa kuwapelekea huduma stahiki katika makaazi Yao kwani imekua ni mkombozi na kuwaomdolea kilio kikubwa ambacho walichokua nacho hapo awali .
Vijiji vya mtakuja mikinduni na mgelele vilivyopo wilaya ya wete ni miongoni mwa vijiji vilivyopelekewa huda ya maji , Barbara ,umeme na kujengewa skuli kutokana na umbali mrefu uliokuepo wa kuzitafuta huduma hizo ambapo kina kaya zaidi ya 35.
Comments
Post a Comment