WIZARA YA AFYA ZANZIBAR IMEWATAKA WANACHI KUTOPUUZA KUSAJILI KADI ZA MATIBABU............ NI MUHIMU
Na Amina Ahmed .
wizara ya afya Zanzibar imetoa wiki mbili kwa wananchi wote ambao hawasajili kadi i za afya ya mtibabu zinazotolewa na wahudumu wa afya jamii katika shehia zao kuharakisha kusajili kadi hizo na kuanza kuzitumia wanapokwenda katika kufata matibabu katika vituo vya afya pamoja na hospitali .
Ametoa Agizo Hilo Waziri wa Afya Zanzibar Dk Nassor Ahmed Mazrui Alipkiwa akizungumza na masheha Wa mkoa wa kaskazini Pemba Katika Warsha maalum ya utoaji taarifa juu ya umuhimu wa kusajili kafi za matibabu kwa wananchi huko katika ukumbi wa Skuli ya Miti ulaya Wete.
Amesema Kadi hizo zinatolewa kwa wananchi kupitia wahudumu wa afya jamii wanaopita katika shehia kusajili vitambulisho vya afya zina lengo la kusaidia serikali kupanga mpango wa utowaji wa huduma za matibabu na urahisi wa kupata huduma za afya zilizo bora kwa wananchi .
Amesema Serikali hairidhishwi n mfumo wa matibabu uliopo kwa sasa hivyo mfumo huo wa ktumia kitambulisho cha matibabu utasaidia wananchi kuweza kupata mtibabu sahihi na kwa wakati
Aidha Waziri Mazrui amefahamisha kuwa mfumo huo utasaidia kujua taarifa muhimu za mwananchi ikiwa ni pamoja na kujua taarifa muhimu za maradhi mbali mbali ya mwananchi.
Kwa upande wake mkurugezi mkaazi kutoka shirika la Pharm Acess Faundation Akses Dr .HERI Marwa amesema MFUMO huo utaweza kusadia kuweka kbmbu za wagonjwa na mahali walipotibiwa hivyo ametaka Wanachi kuzitumia kadi hizo Ili kuweza kapata matbabu bila usumbufu .
Nae mkuu wa wilaya ya wete Dr ,Hamad Omar Bakar amesema mkoa Kwa kushirikiama na Masheha ili kuendelea kwalimisha wananchi Umuhimu wa kutumia kadi za matibabu na watahakikisha wananchi wote wanapata kadi hio bila usumbufu.
mwisho.
Comments
Post a Comment