WIZARA AFYA ZANZIBAR TAYARI IMEANZA KUJIPANGA KUDHIBITI UGONJWA EBOLA KUTOINGIA NCHINI
Na AMINA AHMED
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui Amewatoa hofu wananchi kuhusu ugonjwa wa ebola ambao umeanza kusambaa virusi vyake katika nchi za jirani za Africa ikiemo Uganda ambapo amesema kuwa wizara imeanza kuweka ulinzi katika maeneo ya mipaka yake katika kudhibiti kuingia ugonjwa huo visiwani Zanzibar.
WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR NASSOR AHMED MAZRUI
Akizungumza na Habari hizi waziri huyo amesema kuwa tayari wizara inaendelea kujipanga kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini .
"Tayari Tumeanza kuchukua tahadhari kudhibiti ugonjwa huo endapo utaingia nchini ikiwa ni pamoja na kimarisha ulinzi na kuweka vifaa vya afya ambvyo vitasaidia kupima afya za wanaoingia kutoka nchi nyengine.
Alisema kuwa licha ya kudhibiti katika maeneo hayo lakini pia serikali kupitia wizara hiyo imeeendaa vifaa vya kutosha vya kujikinga madakatari wa kutoa matibabu wa ugonjwa huo endapo utaingia nchini ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo maalum ya kuwaweka wagonjwa endapo watabainika.
"Hatuombi uingie nchini kwetu lakini endapo utaingia Tayari tumeweka vifaa vya kutosha madakatari watakaosaidia kudhibiti kuenea kwa ugonjwa"
Mwisho
Comments
Post a Comment