WAZIRI MASOUD AFANYA ZIARA UJENZI WA BUSTANI MWANAMASHUNGI CHAKE CHAKE.
NA AMINA AHMED MOH’D
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa Serikali Za Mitaa Na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Muhammed Amefanya ziara maalum ya kutembelea na kukagua ujenzi wa eneo la Bustani Mwanamshungi Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba.
Akiwa Katika eneo La ujenzi huo Waziri Massoud Amewataka Wakanadarasi kuongeza kasi ili wananchi waweze kulitumia jengo hilo kwa wakati sahihi uliowekwa na serikali.
WAZIRI TAMISEMI ZANZIBAR. MASSOUD ALI MUHAMED.
Aidha Amewataka wasimamizi kufuatilia na kutembelea ujenzi huo ili kiongeza mashirikiano na kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Eneo hilo la bustani ya kupumzikia wananchi.
Akizungumza mkuu wa wilaya ya chake chake Abdalla Rashid Ali amesema wataendelea kusimamia na kutembelea mara kwa mara kuona ujenzi huo unavyoendelea ikiwa ni pamoja na kupokea changmoto zitakazojitokeza ili kuziptia ufumbuzi.
Ghafla ya kukagua ujenzi huo iliambatana viongozi mbali mbali ikiwa ni pamoja na mkurugenzi wa Baraza la Chake chake, Ofisa mdhamini wizara ya nchi ofisi ya raisi tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz Pemba pamoja na wasimamizi wa mradi huo.
MKUU WA WILAYA YA CHAKE CHAKE ABDALLA RASHID ALI PAMOJA NA AFISA MDHAMINI TAMISEMI PEMBA THABIT OTHMAN ALI.
Mwisho
.
Comments
Post a Comment