WAZAZI WAASWA MASHIRIKIANO KUTIMIZA NDOTO ZA WATOTO.
Mahafali ya kwanza Ya wanafunzi wa wahitimu wa Darasa la awali ( Maandalizi ) Pamoja Madarasa ya Msingi nSuper kutoka Skuli ya The Bright Academy Yaliojulikana kama Super Heroes days amefanyika leo katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba .
Akizungumza katika maghafali hayo Ofisa mdhamini Ofisi ya Rais Ikulu Pemba Shuweha Abdalla Omar amesema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi binafsi za kukuza elimu nchini kwa kutatua changamoto mbali mbali zinazokabili taasisi hizo ambazo hupelekea kurudiaha nyuma harakati zao.
SHUWEHA ABDALLA OMAR
OFISA MDHAMINI OFISI YA RAIS IKULU PEMBA
Amesema mchango unaofanywa na taasisi za elimu ikiwemo kituo hicho cha the bright academy ni mkubwa katika sekta ya elimu hivyo serikali haitosita kuwaunga Mkono katika kuleta mendeleo na mageuzi ya elimu.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya nane inaendelea kuchukua jitihada mbali mbali kuboresha mendeleo ya elimu ikiwa ni pamoja na kujenga skuli za kisasa zitakazosaidia kuboresha elimu kwa wanafunzi sambamba na kuruhisiwa wanafunzi kutumia skul hub kujiendeleza.
Bi Shuweha Aliwapongeza waalimu wa skuli hiyo kwa jitihada zao katika kusimamia vyema wanafunzi ambapo pia amewataka wazazi kujitahidi kulipa ada kwa wakati sambamba kuwahimiza watoto kusoma kwa bidii pamoja na kufika kwa wakati.
Aidha Mdhamini huyo amewapongeza wahitimu hao kwa jitihada zao walizozionesha katika masomo ambapo amewaasa kuendeleza bidii katika kujifunza mambo mbali mbali wanayofundishwa.
Akizungumza na wanafunzi wazazi pamoja na wahitimu wa mahafali hayo Mweyekiti wa baraza la vijana taifa Rushda Khamis Kassim amewaasa wazazi na wanajamii kusimamia ndoto za watoto walizonazo na kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji ambao unaendelea kuathiri watoto na kupelekea kukatisha malengo yao.
RUSHDA KHAMIS KASSIM.
M/KITI BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Abdul karim Yunus Yahya ambae pia ni mwenyekiti wa vituo vya elimu za kujtegemea Zanzibar amesema kuwa licha ya kupiga hatua kwa kituo hicho ikiwa ni pmoja na kupata usajili rasmi sambamba na kuwa kituo bora kinachoongoza kwa kutoa elimu bora lakini pia kinakabiliwa na ukosefu wa jengo jambo ambalo linarudisha nyuma kutokana na kulipia kodi ya jengo kila mwezi kuendeleza shughuli hizo.
Aidha Mkuu huyo amewaomba wadau na wahisani wa maendeleo ya elimu kusaidia ujenzi wa kituo cha the bright ambao tayari kwa hatua za awali umeanza ili kuondokana na changamoto ya kukosa eneo lao wenyewe.
MWALIMU MKUU KITUO CHA THE BRIGHT ACADEMY
Sherehe ya Mahafali hayo imeambatana na burudani mbali mbali kutoka kwa wanafunzi wa kituo hicho ikiwa ni pamoja na burudani ya musiki, kaswida, Mashindano ya kula, masuali ya papo kwa papo kwa lugha ya kiengereza, kuongea lugha ya kiengereza kwa ufasaha kwa watoto , utenzi, elimu y vitendo ambapo ktika mahafali hayo ya super heroes kids day uliimba wimbo wa taifa ikiwa ni katika kumuenzi baba wa taifa hayat Julius Nyerere katika kukumbuka na kuthamini mchango aliouacha kwa taifa la Tanzania.
WANAFUNZI THE BRIGHT KIDS
MATUKIO YA WANAFUNZI KATIKA MAHAFALI YA THE BRIGHT ACADEMY SUPER HEROES KIDS.
PICHA BAADHI YA WANAFUNZI
PICHA MWAAFUNZI
Mwisho.
Comments
Post a Comment